26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Shaka awashia moto vyama vya upinzani

Mwandishi wetu-Ulanga



KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, amevitaka vyama vya upinzani nchini kujipima kisiasa, kutafakari na kujitathmini hatimaye vibaini udhaifu wao kwa kujua kwa nini viongozi wake wakiwamo wabunge, madiwani na hata wanachama wa kawaida wanavihama na kujiunga na CCM.

Ameyasema hayo leo alhamisi Novemba 22, 2018 Wilayani Ulanga, wakati akimkaribisha Mjumbe wa NEC, Hassan Bantu,  kwa ajili ya kuwapokea viongozi na wanachama wa vyama upinzani waliorudisha kadi zao na kujiunga na CCM.

Amesema CCM ilitumia muda mwingi kutafakari, kujitathmini na kujipima kwanini kumekuwepo na shutuma dhidi ya serikali na watendaji wake hatimaye kikapata majawabu ambayo yakawafanya wajipange, kutekeleza na kuchukua hatua .

“Yapo mambo CCM iliyabaini na kuanza kuchukua hatua haraka .Tuliona kuna ombwe la kukosekana tunu ya utendaji na ufanisi. Kulikithiri vitendo vya rushwa na ubadhirifu. Mmongonyoko wa maadili, ufisadi na kupungua nidhamu ya kazi,” amesema Shaka

Aidha amesema CCM haikutafuata mchawi wala viongozi wake kunyoosheana vidole vya lawama , badala yake iliposema ni lazima walikubali kujikosoa, kujivua gamba, kukomesha ufisadi, rushwa na usaliti.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles