25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Shaba, Kipanga, Chuoni hatihati Ligi Kuu

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
LIGI Kuu ya Zanzibar inatarajia kumalizika Juni 3, mwaka huu, huku timu za Shaba, Kipanga, Chuoni, Malindi na Miembeni zikiwa katika hatari ya kushuka daraja.
Miembeni na Malindi zina pointi 23 kila moja na zimebakiwa na michezo miwili, huku Kipanga ikiwa na pointi 20 na mchezo mmoja mkononi, Shaba na Chuoni zina pointi 19 kila moja na wamebakiwa na michezo miwili kila mmoja.
Hadi sasa timu ya Mafunzo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 39 kwa kucheza mechi 20 na kusaliwa na mechi mbili, wakati JKU wao wanashika bafasi ya pili wakiwa na pointi 38 katika mechi 20 walizocheza, wakibakiza mechi mbili pia.
Nafasi ya tatu inashikwa na Hardrock, yenye pointi 29 katika mechi 21 ilizocheza na imesalia mechi moja.
Mafunzo imebakiza mechi dhidi ya Polisi Mei 24, mwaka huu na itamaliza na Miembeni Juni 3, huku JKU ikisaliwa na mechi na Chuoni, ikimaliza na Polisi Mei 28.
Hata hivyo, Zimamoto yenye pointi 28, inaweza kuishusha Hardrock katika nafasi ya tatu ikiwa itashinda mechi yake dhidi ya Mtende Rangers, itakayochezwa Mei 26, mwaka huu, kwani wana pointi 28 kwa mechi 20 walizocheza na wamebakiwa na mechi mbili.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles