24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yazindua programu yakuimarisha ufugaji nyuki

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Seriikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua program ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki katika mikoa mitano nchini itakayogharimu Sh bilioni 27 katika utekelezaji wake.

Programu hiyo itaenda kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa mazao ya nyuki, kuwezesha maeneo ya uchakataji na uongezaji wa thamani wa mazao ya nyuki,kujenga uwezo wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufugaji nyuki pamoja na taasisi zinazosimamia sekta hiyo.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 21,2022, jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Programu hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa asali nchini uliongezeka kutoka tani 4,860 mwaka 1998  za asali hadi kufikia tani 31,179 mwaka 2021 na nta kutoka 1834 mwaka 1998 hadi tani 1894 mwaka 2021.

Amesema kiwango hicho bado ni kidogo ukilinganisha na fursa ya uzalishaji wa asali nchini ambapo amedai kama nchi kuna fursa ya kuzalisha asali takribani tani 138,000 na tani 9200 za nta kwa mwaka.

Akizungumzia Programu hiyo ya miaka mitano, Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa inafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na itatekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Singida, Shinyanga na Pemba.

Amesema programu hiyo itajenga uwezo wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufugaji nyuki pamoja na taasisi zinazosimamia sekta hiyo ya ufugaji wa nyuki.

Naibu Waziri huyo amesema  kuwa program hiyo itakwenda kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa mazao ya nyuki, kuwezesha maeneo ya uchakataji na uongezaji wa thamani wa mazao ya nyuki.

Naibu Waziri huyo amesema programu hiyo itawezesha taasisi ya utafiti wa nyuki kuweka vitendea kazi katika maabara ya utafiti wa nyuki iliyopo Njiro mkoani Arusha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Francis Michael amesema  program hiyo itawezesha kuboresha mifumo mbalimbali ya kibiashara ili kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wa mazao ya nyuki.

“Itaimarisha na kukuza ujuzi kwa watoa huduma za kibiashara na kuboresha uwezo wa wachakataji, wasindikaji na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki ili waweze kusimamia, kukuza na kusafirisha mazao yao hayo,”amesema Michael.

Naye, Balozi wa Umoja wa Ulaya, Manfredo Fanti amesema soko la asali kwa nchi za Ulaya ni kubwa na bado wanahitaji kiasi kikubwa kutoka Tanzania.

Amesema hiyo ndiyo sababu ya kuwekeza fedha nyingi katika sekta hiyo ambazo ni msaada na siyo mkopo.

Amesema kuwa hakuna kiwango kamili kinachotakiwa kupelekwa huko isipokuwa ubora wa asali ndiyo utakuwa kigezo cha kutazamwa na watu wa Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles