26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SERIKALI YAWATIA KITANZI WAKURUGENZI MWANZA

Na BENJAMIN MASESE

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, amesema atazichukulia hatua halmashauri za Mkoa wa Mwanza ambazo zitasababisha deni jipya katika sekta ya ardhi kwa kutwaa maeneo ya wananchi bila fidia.

Amesema Serikali  imekwisha kutoa agizo kwa halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai mosi mwaka huu, hakuna ruksa ya kutwaa eneo la mwananchi bila fidia.

Alisisitiza kuwa maeneo ambayo yalipimwa na kufanyiwa uthamini kwa matumizi ya umma  na kushindwa kulipwa fidia ndani ya miaka miwili, yanapaswa kurudishwa kwa wamiliki wa awali au kufanya uthamini upya.

Kauli hiyo aliitoa  katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa.

Alishangazwa na kitendo cha wataalamu wa idara ya ardhi kutokuwa na mikakati ya kuzuia ujenzi wa makazi holela.

Akiwa Sengerema   Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mafuru Magesa   alisema mwaka 2016. 2017 zilitolewa hati 197 kwa wananchi na zimekusanywa Sh milioni 217 zinazotokana na kodi ya ardhi.

Alisema mpaka sasa vimepimwa viwanja 5437 ambavyo vinatarajiwa kutolewa hati.

Hata hivyo alisema  wanashindwa kuendelea kupima maeneo mengine kutokana na   migogoro ambayo huchukua muda kumalizika kwa sababu ya kufungua kesi katika baraza la ardhi.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Kipole alisema  baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kuwatumia waganga wa kienyeji katika migogoro ya ardhi na kufikia kuuana kwa njia za ushirikiana ma kujichukulia sheria mkononi.

Akiwa Buchosa,   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Crispin Luanda alisema vimekwishakuoimwa  na kupima viwanja tisa   pekee tangu ilipoanzishwa   Novemba, 2015.

Naibu Waziri aliwatahadhirisha wakurugenzi wa halmashauri hizo kwamba atakayesababisha deni jipya katika sekta ya ardhi, anapaswa kutambua anajiweka katika wakati mgumu katika nafasi yake.

“Hapa Sengerema takwimu zinaonyeshwa ilianzishwa mwaka 1975 lakini hadi leo eneo la wilaya halijapimwa.

“Kibaya zaidi hata mpango wa matumizi bora ya ardhi haupo sasa kinachosubiriwa ni migogoro, watumishi mpo ofisini lakini hakuna mnachofanya.

“Nimekuwa nikitoa maagizo mengi cha kufanya lakini ninaporudi nakuta mambo ni yale yale, mnadhihirisha mnafanya kazi kwa mazoea.

“Sasa nawajulisheni kwamba ole wenu muanzishe deni jipya, hakuna kutwaa eneo la mwananchi bila fidia.

“Kama hamna uwezo wa kulipa fidia, nendeeni mkazungumze na wenye maeneo mpime viwanja mgawane kwa asilimia na muwape hati miliki.

“Sitaki kusikia mnazalisha deni, na yale maeneo ambayo mliyapima na kushindwa kulipa fidia ndani ya miaka miwili, tambueni wananchi wana haki ya kuyaendeleza,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles