27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawaonya wanaokeketa wasichana

Na TIMOTHY ITEMBE

SERIKALI imewaonywa wazee wa  mila na wakazi wa Wilaya ya Tarime kuwa yeyote atakaebainika kukeketa mtoto wa kike atachukuliwa hatua kali.

Hatua hizo ni pamoja na  kushtakiwa kwa kutenda ukatili ili liwe fundisho kwa wengine.

Onyo hilo lilitolewa  na Mkuu wa Wilaya Tarime mkoani Mara, Glorius Luoga wakati akifungua semina ya siku moja iliyoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa udhamini wa Shirika la  Faundation For Civil Socierty.

Luoga alisema kuendelea  vitendo vya ukeketaji kumekuwa kukitokana na kutochukuliwa  hatua wahusika.

Alionya kuwa sasa atasimamia kuhakikisha hatua zinachukuliwa vilivyo  kukomesha jambo hilo ambao limekuwa likiharibu sifa ya wilaya hiyo kwa muda mrefu.

“Kila siku Serikali kwa kushirikiana na mashirika wamekuwa wakitoa elimu kwa wadau pamoja na wazee wa mila kuzuia na kukomesha ukeketaji.

“Sasa kwa kuwa huko nyuma kulilegalega sasa nawaeleza yeyote atakayebainika akimkeketa mtoto wa kike atachukuliwa hatua kali za sheria ikiwamo kukamatwa na kupandishwa mahakamani kujibu mashtaka,” alisisitiza.

DC alitumia fursa hiyo kuwataka wazee wa mila kusimamia mchakato wa kukomesha mila hiyo na kuwaasa wanajamii kuwapeleka watoto wa kiume kufanyiwa tohara hospitalini kitaalamu badala ya zile za kimila ambazo ni hatari kwa maisha ya watoto wao.

Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Coshuma Mtengeti, alisema  kila watoto wawili waliochini ya umri wa miaka 18 mmoja kati yao anakeketwa.

Coshuma alisema  lengo la mradi wa kukuza haki za mtoto wa kike ni kuutambulisha mradi, msimamo wa serikali kuhusu kukomesha ukeketaji kuwajengea uwezo wadau juu ya madhara ya ukeketaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles