27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATUMIA MILIONI 50 KUWAFUKUZA NDEGE PORI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Na BENJAMIN MASESE, 

SERIKALI inalazimika kutumia Sh milioni 50 kwa mwaka kuwalipa wafanyakazi 35 wa Uwanja wa Ndege   wa Mwanza kuwafukuza ndege hai ili kuepuka kuingia kwenye injini ndege inapotua au kuruka.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Meneja wa uwanja huo, Easter Madale, wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Waziri alikuwa akikagua ujenzi wa miundombinu jengo la mizigo, mnara wa kuongozea ndege, uhamishaji wa mto na uongezaji wa urefu wa mita 500 za njia ya kurukia ndege.

Madale alisema katika uwanja huo wanakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo kutokuwa na uzio, kitendo ambacho kinatoa mwanya kwa adui kuingia muda wowote.

Alishukuru kuwapo kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambayo askari wamekuwa katika doria za mara kwa mara kuzungukia uwanja huo.

“Pia kuna changamoto ya ndege hao ambao wamewahi kuleta madhara ya kuingia kwenye injini ya ndege na kuanguka.

“Kama uongozi tumekuwa na mipango ya aina mbalimbali ya kupata suluhisho la ndege hai, hivi sasa tunatumia wafanyakazi wapatao 35 kuwafukuza, hasa  ratiba inapoonyesha ndege inahitaji kutua au kuruka.

“Hawa watumishi kila mmoja analipwa Sh 150,000 kwa mwezi na kwa mwaka tunatumia Sh milioni 50 kuwalipa mishahara ya kazi hiyo.

“Nchi nyingine zimekuwa zikitumia njia mbadala ya kutumia bunduki za milio na baadhi ya vifaa vya kutoa sauti, lakini hawa ndege hai wakishazoea milio hiyo hawaondoki.

“Bado tunaendelea kujifunza teknolojia za nchi nyingine wanazotumia kuwafukuza ndege hai ili tusije kuiga jambo ambalo pengine likatuingiza kwenye gharama, huku mafanikio yakiwa hayapo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles