24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATOA BILIONI 7.6/ UWANJA WA NDEGE MWANZA

Profesa Makame Mbarawa
Profesa Makame Mbarawa

Na BENJAMIN MASESE,

SERIKALI imeilipa Sh bilioni 7.6 Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) inayojenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza, huku ikitoa miezi minane ikabidhi jengo la mnara wa kuongezea ndege na ofisi za watumishi.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Mwanza jana na Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi  na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua  ujenzi wa miundombinu ya uwanja wa ndege, upanuzi wa barabara na ujenzi wa daraja la Furahisha.

Profesa Mbarawa alisema ujenzi huo ulikuwa umesimama tangu mwaka 2014 kutokana na mkandarasi wa Kampuni ya BCEG kuidai Serikali Sh bilioni 7.6.

Fedha hizo ni kati ya Sh bilioni 105 zinazohitajika kujenga jengo la mizigo, mnara wa kuongozea ndege, kuhamisha mto na kuongeza urefu wa mita 500 eneo la kurukia ndege.

“Mtakumbuka nilikuja hapa Septemba 14, mwaka huu kufanya ziara na nilianzia hapa uwanja wa ndege.

“Nilikuta ujenzi umesimama kwa sababu ya Serikali kudaiwa, leo nimerudi tena kuwahakikishia kwamba Serikali ya awamu ya tano haina mchezo, nimekuja na fedha na tayari tumemlipa mkandarasi.

“Ninachotaka kuanzia sasa kazi ifanyike kwa haraka, nilitaka kutoa miezi sita, lakini nasema ifikapo Agosti mwakani nataka  tukabidhiwe, vinginevyo Kampuni ya BCEG ijiandae kutulipa faini ya kuchelewesha,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles