27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

MTOTO WA RAIS GUEBUZA AUAWA KWA RISASI

d1mcnux

MAPUTO, MSUMBIJI

MTOTO wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Armando Guebuza, ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Maputo.

Valentina Guebuza, mwenye umri wa miaka 36 ameripotiwa kupigwa risasi mara kadhaa nyumbani kwake na kufariki dunia kutokana na majeraha wakati akipelekwa hospitalini.

Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Msumbiji, mume wa binti huyo, Zofino Muiuane, alikamatwa na polisi katika moja wapo ya maeneo ya burudani mjini Maputo kufuatia tukio hilo lililotokea juzi.

Valentina aliorodheshwa nafasi ya saba miongoni mwa wanawake chipukizi wenye ushawishi barani Afrika na jarida la Forbes mwaka wa 2013.

Alishikilia nafasi ya juu katika kampuni kadhaa za mawasiliano pamoja na biashara zinazomilikiwa na familia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles