28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa matumaini Mabadiliko Sheria ya Habari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema, mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia sekta ya habari nchini, umefika hatua nzuri.

Msigwa ametoa kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi wa habari hii, hatua iliyofikiwa baada ya kikao cha wadau wa habari na serikali cha Agosti 11na 12 mwaka huu.

Akijibu swali hilo kwa ufupi, Msigwa amesema mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari unaendelea na upo katika hatua nzuri ndani ya serikali.

“Subirini, muwe na Subira mtajulishwa hatua lakini mpaka sasa mchakato unakwenda vizuri,” amesema Msigwa na kusisitiza kwamba, serikali itatoa taarifa yah atua zinazoendelea.

Kabla ya kutafutwa Msigwa, mwandishi aliwasiliana na Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhusu mchakato huo.

Nape alimwekeza mwandishi kupata ufafanuzi kutoka kwa Msemaji wa Serikali (Msigwa). “Mtafute Msigwa, akaueleza,” alisema Nape.

Mchakato wa mabadiliko ya sheria zinazominya uhuru wa habari nchini, ulishika kasi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza serikali na wadau kukaa Pamoja na kuangalia namna ya kumaliza kero hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles