25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yashauriwa kuunda mtaala kwa wasiosikia

Lessly Nyambo
Lessly Nyambo

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

SERIKALI imeshauriwa kuunda mtaala utakaotumika kuwafundisha watoto wenye ulemavu wa kusikia kuliko ilivyo sasa.

Mtaala uliopo sasa unawataka walimu wa wanafunzi hao kuwafundisha kama vile wanavyofundishwa wale wasiokuwa na ulemavu huo.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mary Urassa wa Shule ya Msingi Msasani A alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mwalimu huyo ambaye anafundisha Kitengo maalumu cha viziwi shuleni hapo alisema kuendelea kutumika kwa mtaala mmoja ni jambo linalowapa changamoto watoto na kushindwa kujifunza vitu vingi.

“Watoto hawa wamegawanyika kuna ambao ukimfundisha anakuwa mwepesi Kuelewa lakini wapo ambao ni wazito kidogo kuelewa lugha ya alama.

“Sasa tunapewa mtaala mmoja na wale wasiokuwa na ulemavu, inakuwa changamoto kubwa kwao hasa wale wenye uelewa mdogo kujifunza sambamba na wenzao,” alisema.

Mkuu wa Kitengo hicho,  Lessly Nyambo alisema watoto wenye ulemavu wa kusikia huwa hawapendi kupewa vitu vingi ili waweze kujifunza.

“Wengine hata vitabu ukiwapa hawapendi,  wanapenda vitu vichache vya kuwasaidia na utashangaa kuitumia njia wanayoitaka wanakuwa wepesi kuelewa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles