31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapiga ‘stop’ matumizi ya magogo

Dk. Binilith Mahenge
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge

Na Mauli Muyenjwa, Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge, amewataka wawekezaji wote nchini kuhakikisha wanaacha kutumia magogo katika uzalishaji na badala yake watumie teknolojia ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya tabia ya nchi na uchafuzi wa mazingira.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, katika ziara yake ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia (BIDCO) kilichopo Mikocheni.

Kutokana na kiwanda hicho kuendelea kutumia magogo, Dk. Mahenge, ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya magogo kwani yanaathari kubwa sana kwa jamii.

Waziri huyo alisema kila wakati atahakikisha anatembelea kiwanda hicho ili kuangalia kama wameacha kutumia magogo ndani ya miezi sita na endapo watabainika wanaendelea kutumia magogo hatua kali itachukuliwa dhidi ya kiwanda hicho ikiwemo kufungwa.

“Wawekezaji wa viwanda vingine igeni mfano wa kiwanda cha Coca Cola katika utunzaji wa mazingira, kwani wao ni mfano mzuri kwa viwanda vingine kwa kuanzisha teknolojia nyingine ya kuchunguza maji taka kama ni salama kwa viumbe hai.

“Tunawapenda wawekezaji lakini ni wale wanaotunza na kuyaenzi mazingira kwa usalama wa wananchi na nchi yetu kwa ujumla,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles