32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapata bilioni 400/- Mauzo ya tumbaku 2017/18

NA ALLAN VICENT 

MAUZO ya   tumbaku  nchini yameiwezesha serikali kupata zaidi  ya Sh bilioni 400   mwaka 2017/2018.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Japhet Hasunga katika hafla maalumu ya ufunguzi wa masoko ya zao hilo kwa msimu wa 2019/2020 yaliyofanyika  wilayani Urambo.

Alisema     tumbaku pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali bado  inatoa mchango mkubwa  katika pato la taifa kwa kuingizia serikali fedha nyingi za kigeni.

Waziri alisema  zao hilo ni mkombozi kwa uchumi wa taifa kwa vile  linashika nafasi ya pili kwa kuingiza mapato mengi.  

 Hasunga alitaja zao la korosho kuwa ndilo linaloongoza kwa

kuiingizia serikali mapato mengi zaidi ya fedha za kigeni ikizingatiwa katika msimu wa 2017/2018 mauzo yake yaliingiza Dola za Marekani milioni 526.

Alitaja zao la tatu kuwa ni kahawa kwa kuingiza Dola za Marekani milioni 126.1, huku mengine yakiwa ni chai iliyoingiza Dola za Marekani milioni 49,  pamba Dola za Marekani milioni 36.6, karafuu  Dola za Marekani milioni 54.6 na mkonge Dola za Marekani milioni 28.9.

Waziri alisema  zao la tumbaku pamoja na kuingiza fedha nyingi za kigeni limekuwa likipungua katika uzalishaji.  

Alieleza kuwa kwa mwaka 2010/11 tumbaku ililimwa kilo milioni 126 na kushuka hadi kilo milioni 54.8 kwa mwaka 2018/19.

Alisisitiza kuwa kilimo cha tumbaku kinapaswa kuendelea kupewa kipaumbele na msaada unaotakiwa   kuwanufaisha wakulima, lakini ili kupata mafanikio hayo ni lazima walime kwa tija.

Waziri Hasunga aliagiza tumbaku yote iwe imenunuliwa ifikapo Julai mwaka huu.

Alisisitiza kuwa hicho ndiyo kigezo mojawapo cha

kuthibitishwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku,   Dk. Julius Ningu.

Naye Dk Ningu alisema  bodi yake itahakikisha zao hilo linaendelea kufanya vizuri katika soko la kimataifa kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Alisema kwa miaka 10 mfululizo zao hilo limekuwa likiongoza

ingawa mwaka jana limepitwa na korosho lakini wamejipanga kuendelea kuongoza huku mkoa wa Tabora ukiwa kinara kwa kuzalisha asilimia 61 ya tumbaku yote inayozalishwa  nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles