31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Gesi asili yasambazwa Mtwara, Lindi, Pwani, Dar

NA RAMADHAN HASSAN, Dodoma

SERIKALI imeanza kutekeleza mradi wa kusambaza gesi asilia katika miji ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam ikiwa ni nishati mbadala   kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu Mgalu aliyasema hayo  bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Ally Ungando (CCM).

Alisema pia kuwa Mei 18 mwaka 2018 serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ilisaini mkataba na Kampuni ya Mihan gas kwa ajili ya kusambaza vifaa vya kupikia mitungi ya gesi na majiko kwa watumishi wa umma na wananchi wengine,  mpango   unaolenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.

Katika swali lake, Ungando  alihoji Serikali inamkakati gani wa kupeleka nishati mbadala katika Jimbo lake ikiwa ni pamoja ni aina  gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa.

Mbunge huyo alisema  wananchi wanaoishi katika Jimbo la Kibiti hutumia   kuni kwa matumizi ya nyumbani, shuleni, gerezani hivyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti hovyo .

‘Je serikali inamkakati gani wa kupeleka nishati mbadala? Na je ni aina gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa?” aliuliza Ungando.

Akijibu, Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu, alisema  Mei 18 mwaka 2018 serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ilisaini mkataba wa kampuni ya Mihan Gas kwa ajili ya kusambaza vifaa vya kupikia mitungi ya gesi na majiko kwa watumishi wa umma na wananchi wengine   mpango  unaolenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.

 Mgalu alisema   Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 imetoa muongozo wa kuboresha maisha ya wananchi kwa matumizi bora ya nishati kupitia teknolojia ya kisasa badala ya kuni na mkaa.

Alisema Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za makusudi kuendeleza vyanzo mbalimbali vya nishati ilikuongeza mchango wa nishati mbadala katika upatikanaji wa nishati nchini.

“Katika kipindi cha muda wa kati kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 serikali inatekeleza miradi ya kuzalisha umeme kupitia vyanzo vya gharama nafuu vya maji na gesi ikiwa ni mkakati wa kuwawezesha wananchi kumudu kutumia nishati ya umeme kwa gharama nafuu kwajili ya kupikia badala ya kuni na mkaa,

“Kwa kuwa sehemu ya kuni na mkaa unaotumika katika Jiji la Dar es Salaam huzalishwa katika Wilaya ya Kibiti hatua ya kwanza kutumia gesi asilia kwa kupikia itapunguza uharibifu mkubwa wa mazingira kupitia ukataji miti ovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa,”alisema Mgalu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles