25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri: Serikali kulipa fidia kutegemea hali ya fedha

SERIKALI imesema inaendelea na mpango wa utaratibu  wa kulipa fidia stahiki za wananchi kadri hali ya fedha itavyoruhusu kwa mujibu wa sheria ya utwaaji ardhi.

Hayo yalielezwa  bungeni jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambile Masoud Salim(CUF).

Katika swali lake Salim alitaka kujua kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi ambao maeneo yao yametwaliwa na jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) pasipo kulipwa fidia .

Salim alihoji Serikali inampango gani wa haraka kulipa fidia kwa wananchi hao.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwinyi alikiri ni kweli yapo maeneo mbalimbali yaliotwaliwa na jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kwajili ya utekelezaji kwa jukumu la ulinzi wa nchi na mipaka yake.

“Baadhi ya maeneo hayo yamelipwa fidia na mengine mchakato wa kulipa fidia kwa wamiliki unaendelea,”alisema Mwinyi.

Alisema kwa mwaka wa fedha 2018/19 wizara ilitenga Sh bilioni 20.9 kwa ajili ya kulipa fidia maeneo yaliotwaliwa na jeshi baada ya uhakiki wa malipo ya fidia tayari Sh  3,005,697,801.00 zimelipwa kama fidia.

Aliongeza kuwa uhakiki wa madai ya fidia unaendelea katika maeneo mengine na   uhakiki utakapokamilika serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa litalipa fidia hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles