23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kutenga fedha za kutosha

Na Tunu Nassor, Dar es Salaam
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wameiomba Serikali kutenga fedha za kutosha kwa taasisi zote za Serikali zinazohusika na suala la kukomesha ukatili dhidi ya albino.
Lengo la kutekeleza programu za kuelimisha umma kuharakisha upelelezi na uendeshaji wa kesi za watu wanaodaiwa kufanya ukatili huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga alisema tume pamoja na wadau walikubaliana kuwa mapambano dhidi ya ukatili na mauaji ya watu wenye ualbino ni suala linalohitaji rasilimali fedha na jitihada za kutosha.
“Tunaiomba Serikali kutenga fedha za kutosha kwa taasisi zote za Serikali zinazohusika na suala hili kwa ajili ya kutekeleza na kuharakisha upelelezi na uendeshaji wa kesi hizo,” alisema.
Nyanduga alisema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ilikutana na wadau mbalimbali wa haki za binadamu, ili kujadili mikakati ya kukomesha ukatili na mauaji yanayoendelea dhidi ya watu wenye ualbino.
Alisema mkutano huo wa wadau kwa pamoja walikemea mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino unaofanywa na watu wenye imani za kishirikina, ambao wanaamini kuwa utajiri na vyeo au madaraka ya kisiasa vinapatikana kupitia matumizi ya viungo vya watu wenye ualbino.
Nyanduga alisema mapendekezo yote yanalenga kutoa ulinzi na huduma za afya kwa watu wenye ualbino nchini. Ushiriki wa jamii katika ngazi zote ni muhimu katika kupata mafanikio katika suala hilo.
Alisema wamependekeza Idara ya Mahakama, Ofisi ya DPP na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ziharakishe na kutoa kipaumbele uchunguzi na upelelezi, mashtaka na usikilizaji wa kesi za mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles