24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuboreshasheria tiba mbadala,asili

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

SERIKALI imeombwa kuendelea kufanya maboresho ya sheria inayohusu tiba mbadala na asili ili kuendana na mazingira yaliyopo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Cornwell Tanzania, Elizabeth Lema alisema  awali sheria ya usajili wa tiba za asili zilikuwa zikikwamisha jitihada za kupata usajili kwa wakati ukilinganisha na hivi sasa.

Aliishukuru Serikali kwa kulipa wepesi suala hilo na kuwezesha baadhi wawekezaji kusajili biashara zao hususani zinazohusiana na tiba za asili na mbadala kuweza kusajiliwa.

“Rais Magufuli mara baada ya kuingia madarakani amewezesha tiba mbadala na Tiba asili kupata usajili ingawa Sheria haibadishwi kwa siku moja,”alisema.

Alisema kwa sababu ya kutokuwa na elimu ya sahihi ya tiba mbadala na asili baadhi ya watendaji Serikalini wamekuwa vikwazo vya upatikanaji usajili  kwa muda muafaka.

Alisema ipo haja ya Serikali kuangalia viwango vya dawa vinavyolingana na mazingira ya nchi yetu tofauti na hivi sasa ambapo vinaangaliwa

Dk.Johnn Brinkmann alisema  kwa sababu ya umuhimu wa dawa hizo, Cornwell Tanzania wameamua kuanzisha chuo kitaachokuwa kinatoa mafunzo ya tiba asili na mbadala na hiyo ni kwa sababu ya kukosekana chuo chenye mafunzo hayo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

“Katika chuo chetu kutakuwa na kozi mbalimbali za muda mfupi ngazi ya astashahada na stashahada na elimu kwa mtu binafsi anayetaka kufahamu masuala ya tiba mbadala au kuangalia afya yake,”alisema.

Alisema sababu nyingine ya kuanzisha chuo hicho,ni kwamba  Tanzania ina miti ya dawa nyingi, inahitaji kuendelea kufanyiwa utafiti na kutumika katika tiba.

“Ipo haha ya kufanya tafiti miti dawa yetu kwa kuwa asilimia kubwa ya miti imeonekana Ina ufanisi mkubwa kiasi kwamba baadhi ya nchi wamekuwa wakifika kuchukua na kwenda kuzifanyia matibabu nchini kwao,”alisema Dk.Brinkmann.

Pamoja na  kituo hicho jana kitaanza kupima bure afya  kwa waTanzania ili waweze kujua Afya zao na kupatiwa matibabu.

Daktari wa kituo hicho, Ralph Brinkmann alishauri kutokana na mfumo wa vipimo unaotumika, vema watu wenye umri wa kuanzia miaka 8 na kuendelea kupata huduma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles