23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Naibu Spika amjulia hali mbowe

Na Mwandishi Wetu

Naibu Spika, Dk.Tulia Ackson leo Jumanne Juni 9, amemjulia hali Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika Hospitali ya Ntyuka jijini Dodoma anakopatiwa matibabu.

Baada ya kumjulia hali Dk. Tulia amesema kuwa amemuona Mbowe akiwa na majeraha mguuni na kwamba wanasubiri taarifa ya daktari ili kujua ameumia kwa kiasi gani.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Ester Bulaya amesema kuwa Mbowe anatarajiwa kusagirishwa muda mchache ujao kwenda Dar es salaam kwa matibabu zaidi.

Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa amesema walimpiga Mbowe walimwambia hawataki kumuua ila wanataka kumuumiza ili ashindwe kufanya kampeni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema Mbowe amepigwa na watu watatu waliomshambulia kwa kutumia mateke na kwamba jeshi la polisi linawasaka watu waliofanya kitendo hicho.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles