31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU yawaonya waandishi wa habari

NA MURUGWA THOMAS, TABORA;

WAANDISHI wa habari wameonywa kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kutumiwa na wanasiasa wasio waaminifu, wakati huu taifa linapojiandaa kufanya uchaguzi mkuu Oktoba, mwaka huu.

Ofisa wa Dawati la Elimu kwa Umma wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora, Edina Adrian aliwataadhalisha  jana wanahabari wasikubali kuhongwa na kutoa taarifaa ambazo si sahihi zinazoweza kuharibu uchaguzi.

Aliwataka kuwa makini ili kutoingia kwenye mtego wa wanasiasa  ambao si waaminifu, bali wafanye kazi zao kwa kuzingatia miiko na maadili ya tasinia hiyo.

Aliwataka watoe elimu kwa wananchi ili waweze kutoa uamuzi ambao ni sahihi kwa kuchagua viongozi wanofaa ili taifa liweze kupata viongozi ambao ni waadirifu na wenye uzalendo na nchi yao.

Alisema waandishi wanapaswa makini ili wasiingie kwenye mtego wa rushwa za wanasiasa ambao sio waaminifu wanaotaka kuwatumia kama ngazi ya kupatia uongozi.

Katika hatua nyingine, taasisi hiyo inatarajia kuwafikisha mahakamani viongozi watatu wa vijiji vya Majogoro na Mwitikio wilayani Sikonge kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa taasisi hiyo Mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo imewataja watuhumiwa hao, kuwa ni Jonas Lughende Mwita (Mwenyekiti wa Kijiji cha Majojoro), Ramadhan Joseph (Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho)na Israel Geoge Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwitikio.

Alisema Mwita na Joseph, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh  810,000 kutoka kwa mkazi mmoja wa kijiji hicho (jina linahifadhiwa) ili wasimchukulie hatua kwa kosa la kuishi na mwizi nyumbani kwake.

Alisema Israel George alikamatwa kwa kosa la kuomba na kupokea hongo ya Sh 200,000 kutoka kwa mwananchi mmoja ili amsaidie kesi yake iliyokuwa inamkabili kwenye ofisi ya serikali ya kijiji hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles