23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuajiri wahitimu wa Vyuo vya Maendeleo

Anna Ruhasha, Mwanza

Serikali imeombwa kutoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu wanaotoka katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo hapa nchini.

Ombi hilo limetolewa katika mahafari ya 22 katika Chuo cha maendeleo ya wananchi Sengerema (FDC) kilichopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza

Aidha, katika taarifa ya chuo iliyosomwa na Mkuu wa Chuo hicho, Hangai Shila imeeleza kuwa kupitia utafiti uliofanywa na chuo hicho kuanzia mwaka 2017 hadi 2020, wamebaini ni wahitimu 102 tu walioajiriwa serikalini ambapo idadi hiyo ni ndogo ikiliganishwa na wingi wa wahitimu katika chuo hicho.

“Sasahivi chuo chetu kinamwitikio wa wanafunzi wengi ukitazama katika usajili wa wanafunzi kwa mwaka 2021 kimesajili washiriki wa kozi mbali mbali 528 ambapo katika mahafari ya leo mgeni rasmi jumla ya wanachuo 151 wamehitimu kati yao wasichana 50 wavulana 101 katika kozi za ushonaji, umeme, useremala, uchomeleaji vyuma, uwalimu wa chekechea.

Akizungumza katika mahafali hiyo Mwakilishi wa Mkurungenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Afsa maendeleo ya jamii, Boniface Kasasilo amesema kuwa serikali kupitia asilimia 10 inayotengwa kwa vijana , wanawake na walemavu inasaidia vijana kujiari kupitia vikundi na maandiko ya kuanzisha miradi ili kuondoa changamoto ya ajira serikalini.

“Nimeona hapa taarifa yenu imebainisha changamoto za ajiri, vifaa vya michezo na vyakujifunzia na kufundishia, suala la ajira lipo wazi kabisa serikali inatoa mikopo kupitia aslimia 10, niwaombe msikae nyumbani bila kazi mkitoka hapa anzisheni vikundi vya pamoja andikeni maandiko ya kuanzisha miradi leteni maombi hayo katika ofisi ya maendeleo ya jamii, mtapewa pesa ambazo hazina liba kwaajiri ya kujipatia vipato,” amesema Boniface

Wakati huo huo ameiomba jamii kutumia vyuo hivyo kwaajili ya kuwapeleka watoto wao kupata elimu mbali mbali za ujuzi wa fani tofauti ili kusaidia kuogeza wataalamu kwenye jamii ambapo ametolewa wanaofunga umeme majumbani asilimia kubwa wanatoka katika vyuo hivyo.

Hata hivyo, baadhi ya wazazi na walezi walioshiriki wameiomba serikali kuboresha mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja nakujega uzio kulingana na kuwa karibu na makazi ya watu hali ambayo siyo salama kwa watoto wao hasa wakike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles