Na SARAH MOSES,DODOMA.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema serikali imeshindwa kuyafutia hati miliki mashamba pori mengi ambayo hayajaendelezwa baada ya kubaini kuwa yamekopewa mabilioni ya fedha katika taasisi za kibenki hapa nchini.
Pia amezitahadharisha taasisi za kibenki nchini kuwa makini kwani endapo itatoa mkopo kwa dhamana ya shamba na likaleta mgogoro kwa kutoendelezwa watakula nao sahani moja.
Ni jukumu la serikali kuhakikisha linalinda umiliki halali kwa watu wenye hati miliki na si kuwanyang’anya mashamba kiholela”alisema Lukuvi.
Alisema wakati wanaendelea na utaratibu huo wa kufuta mashamba yasiyoendelezwa wamebaini kuwa kuna mashamba mengi ambayo yana mikopo katika taasisi za benki hivyo lazima wafuate taratibu ili benki 8 zisije kufilisika.
Hayo aliyasema jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya serikali kuwasilisha taarifa ya ardhi kuhusu hatma ya matumizi ya mashamba makubwa yaliyotelekezwa.