25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa aitaka Serikali kutenga shule za sayansi

Justinian Galabawa
Justinian Galabawa

Na Hadia Khamis-Dar es Salaam

SERIKALI imeshauriwa kuwekeza katika shule za sayansi za sekondari, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwafanya vijana na walimu kuyapenda masomo hayo ambayo yamekuwa yakiwasumbua baadhi ya wanafunzi.

Akizungumza jana Dar es Salaam kando ya mkutano wa masuala ya elimu, Profesa Justinian Galabawa, alisema ni lazima Serikali iangalie utaratibu wa miaka ya nyuma kwa kuwa na shule maalumu za masomo ya sayansi nchini.

Alisema shule hizo zilifanya vizuri na kujipatia umaarufu na kutoa wanafunzi wengi mahiri katika nyanja ya sayansi.

“Serikali ni lazima irudi katika mtindo wa zamani wa kuwa na shule zake za  sayansi,” alisema Profesa Galabawa ambaye ni mwanzilishi wa Shule ya Sekondari Thomas More Machrina ya Dar es Salaam.

Profesa Galabawa alitolea mfano ya shule za sayansi ambazo zilikuwa zikifanya vizuri ambazo ni Pugu, Kibaha na Shule ya wavulana Tabora.

“Kwa mtazamo tu wa kawaida, ni kwamba walimu wa sayansi ni wachache katika shule zetu, na hao wachache pia hawakai,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles