Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Ubora wa Benki ya NMB kiutendaji miaka ya hivikaribuni na mafanikio yake makubwa kifedha mwakajana ni miongoni mwa matokea ya ubunifu na uwekezajikatika mifumo ya kisasa hasa ile ya kidijitali, AfisaMtendaji Mkuu wa benki hiyo, Ruth Zaipuna, amesema.
Akizungumza jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kiongozihuyo alimwambia Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, kuwa mifumo hiyo imekuwa na tija kubwa si tu kwataasisi hiyo kinara wa faida bali pia kwa serikali, wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018, serikali imeweza kukusanya mapato yenye thamani yatakribani Sh trilioni 6 kupitia mifumo hii ambayo pia inamchango mkubwa kwenye ufanisi wa NMB kifedha.
Ruth aliyasema hayo kabla ya kumkabidhi DktMpango hundi ya Sh bilioni 21.8 ambazo NMB imezitoa kwa serikali kama gawio la mwaka 2020 ikiwani ongezeko la asilimia 43 ya kiasi ilichokitoa mwaka2019.
Aidha, pamoja na kuwa mwanahisa mkubwa kwenyebenki hiyo, pia serikali ni mteja mzuri na mdau wakimkakati wa NMB kupitia utekelezaji wa miradimbalimbali.
“Pamoja na miradi hii, uwekezaji ambao Benki ya NMB imeufanya kwenye teknolojia, unaendelea kuiwezeshabenki kuunganisha mifumo yake na taasisi mbalimbaliza serikali na zisizo za kiserikali na hivyo kurahisishaukusanyaji wa mapato,” Zaipuna amesema na kuongeza kuwa:
“Serikali, zaidi ya kuwa mbia, ni mteja mzuri na mkubwawa Benki ya NMB. Sisi tunalitambua hilo natumeendelea kuwekeza katika teknolojia inayotoasuluhisho kwa serikali. Pamoja na kuunganisha mfumo wa malipo ya serikalikatika mifumo ya Benki ya NMB, tunaendelea kuwekezakuhakikisha miamala mingine mbalimbali inafanyika kwanjia ya kielekroniki.
“Juhudi hizi zote zinachangia kuleta ufanisi na pia kupunguza gharama za uendeshaji katika ukusanyaji wamapato. Kwa miaka mitatu, 2018/20, jumla ya Sh trilioni 5.9 zimekusanywa kupitia mifumo ya Benki ya NMB,” amesema.