25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kafulila: Msiende ‘kujimwambafai’

Na Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amewataka wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kwenda kufanya kazi katika maeneo yao bila yakutumia nafasi zao vibaya au kuonyesha nguvu walizonazo na viongozi wenzao.

Kafulila amesema hayo leo Jumatatu Juni 21, 2021 wakati akiwaapisha wakuu hao wa wilaya, ambapo amewataka kutambua kuwa nafasi waliyopewa kubwa na hawatakiwi kumwangusha rais aliyewateua na badala yake wakatumikie wananchi.

“Msiende mkaanza kutunishiana nguvu na viongozi wengine mtakaowakuta, awe mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri au Mkurugenzi, huu sio wakati wa kila mmoja kuanza kuonyeshana nguvu yake, haitapendeza rais aelezwe kuwa kuna ,kuu wa wilaya na mkurugenzi hawaelewani,” amesema Kafulila na kuongeza kuwa;

“Kama wewe ni mkuu wa wilaya tunajua nguvu yako, mkurugenzi tunajua tu, mwenyekiti wa halmashauri tunajua nguvu yako, haina haja ya kwenda uko na kila mtu kutaka kumuonyesha mwenzake nguvu yake, tunachotaka ni kazi basi,” ameongeza Kafulila.

Aidha, Kafulila amewataka viongozi hao kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na siyo kuanza kuwanyanyasa na kutumia madaraka yao vibaya.

Aidha ameongeza kuwa mkoa wa Simiyu umeweka mikakati ya kuboresha kilimo cha pamba, ambapo amewataka wakuu hao wa Wilaya kwenda kupambana na watu wanaofanya shughuli za umachinga kwenye zao hilo.

Mbali na hilo Kafulila amewataka viongozi hao kuhakikisha changamoto zote ambazo wananchi zinawakabili na viongozi hao wana uwezo wa kuzitatua, kuhakikisha wanafanya hivyo na kuhakikisha wanazimaliza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Busega, Gabriel Zakaria amemshukuru Rais Samain kwa kumteua, ambapo amesema kuwa atakuwa kiongozi mwaminifu na anayekwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

“Sitakuwa kiongozi wa kupandisha mabega, naenda kuwa kiongozi wa kushirikiana na kila mmoja, katika kuhakikisha changamoto za wananchi tunazitatua kwa wakati kama ambavyo tumeelekezwa na viongozi wetu,” amesema Zakaria.

Kwa upande Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa, Shemsa Mohamed amewataka viongozi hao, kuhakikisha wanakwenda kutekeleza ilani ya chama hicho huku akiwa pamoja na kuhakikisha wanatatua changmoto zolizoko kwenye maeneo yao ya kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles