NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM
WAKATI mjadala wa kuhusu kikokotoo kipya cha mafao ya kustaafu ukiwa umeshika kasi katika maeneo mbalimbali, Serikali imekubali kukutana na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini ili kujadiliana zaidi kuhusu suala hilo.
Kauli hiyo imetokana na uamuzi uliofanywa na Serikali juu ya malipo ya wastaafu ambapo kikokotoo kinaelekeza kulipwa asilimia 25 ya mafao kwa mkupuo na asilimia 75 iliyobaki italipwa kwa kipindi cha miaka 12.5.
Akizungumza jana alipofanya ziara katika ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Osha), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, alisema mazungumzo hayo ni matokeo ya barua iliyowasilishwa ofisini kwake na viongoziwa vyama hivyo wiki hii ambapo wahusika wameeleza nia yao ya kutaka kukaa nayemeza moja ili kuzungumzia suala hilo.
“Tumekubaliana kukutana kuzungumzia suala la kikokotoo, lakini mazungumzo yetu na makubaliano tutakayoingia tutahakikisha hayakinzani na sheria na taratibu za mifuko yajamii zilizowekwa,” alisisitiza Jenista.
Alisema mazungumzo hayo pia yataangalia makubaliano ya kikao chaawali ambacho kilihusishwa Serikali na Tucta pamoja na wawakilishi wengine.
Alisema mabadiliko yaukokokotoaji wa masuala ya mafao yanapaswa kufuata sheria na taratibuzilizowekwa.
KUHUSU ZIARA
Akizungumzia kuhusu ziara yakekatika ofisi za Osha, Jenista alisema lengo la kutembelea ofisi hizo ni kufuatilia kwa ukaribu utendaji wao ambao unalenga zaidi katika kuwasaidiawafanyakazi kufanya kazi katika sehemu salama.
“Hawa kazi yao ni kuwalindawafanyakazi nchini, kuzuia magonjwa yanayotokana na kazi, kuangalia wafanyakazikutoingia katika migogoro ya kiafya, zote hizi ni kazi zao ambazo ofisi yanguinapaswa kuzifuatilia kwa ukaribu,” alisema Jenista.
Pia aliitaka ofisi hiyo kufanya tathmini kuhusu tozo mbalimbali wanazotoza kwa kuwa kumekuwa na malalamiko ndani ya taasisi mbalimbali ya kwamba tozo hizo ni kubwa sana.
Kwa upande wa Kaimu Mtendaji Mkuuwa Osha, Hadija Mwenda, alisema ujio wa waziri huyo katika ofisi yake unaonyesha wazi kuwa kazi wanazozifanya zina umuhimu mkubwa katika jamii.
Alisema kwa kuzingatia hilo, ofisi yake imejipanga vizuri kuhakikisha wafanyakazi wanafanya shughuli zao katika mazingira mazuri bila bugudha.