26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Uchunguzi mkubwa benki zote nchini

Bakari Kimwanga – Dodoma

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, amesema wako mbioni kuanza ukaguzi wa wafanyakazi wa benki zote nchini.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kupata wafanyakazi wakiwamo wakurugenzi wa benki hizo walio waaminifu na watakaokuwa na uwezo wa kulinda fedha za wateja wadogo.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dodoma alipokuwa akifunga mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha yaliyofanyika Benki Kuu tawi la Dodoma.

Alisema BoT imebaini huko nyuma fedha za wateja wadogo zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye baadhi ya benki ziliibiwa kwa njia za ujanja na wafanyakazi wa benki hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Ili uwe kiongozi mzuri kwenye benki lazima uwe mwaminifu nandio maana BoT sasa tunakwenda kufanya uhakiki wa benki zote nchini. Kwa maana hiyo hii ‘staff auditing’ (ukaguzi wa wafanyakazi) sasa tutakwenda kupata wafanyakazi sahihi ambao watakuwa waaminifu na wakati wote watalinda fedha zawateja na si hilo tu na hili tutalifanya hata kwa viongozi ambao wataongoza benki hizo.

“Na hawa ambao tutawafanyia ‘vetting’ ni lazimawahakikishe wanadhibiti vitendo ambavyo vinajenga picha mbaya kwa wananchidhidi ya benki. Huko nyuma umefanyika ujanja mwingi, unaona taarifa kuwaaliyekopa anamiliki ghorofa lakini ukienda kwenye nyumba unakuta iko katikati ya mto.

“Hili lilikuwa linafanywa sana tena na wafanyakazi wa benki na wengine ilifika mahali huenda hata nanyi (waandishi) walikuja kwenu kuwaambia kama unataka mkopo fungua akaunti ukimwambia sina hela, anakwambia hiyo hakuna neno wanafungua akaunti wanakupa mkopo wa milioni 50 anachukua milioni 20 ukija ukifanya uhakiki kumbe hata aliyepewa alikuwa hajui kitu hata namna ya matumizi ya mkopo.

“Sasa BoT imejipanga kwa kila hali kuhakikisha tunalinda haki za wateja ikiwamo kulinda fedha zao kwenye mabenki, tunajua kilakitu na huko nyuma wengine walioshiriki mchezo huu wapo viongozi wa benkikutoka nje.

“Na walipofanya haya waliondoka na huku nyuma kuacha kilio. Sasa BoT tunawachuja viongozi na wafanyakazi wa benki zote,” alisisitiza Gavana Prof. Luoga.

Profesa Luoga, alisema huduma za kifedha ni muhimu hivyo BoT  inataka imfikie kila mwananchi bila kikwazo.

“Kwa sasa tunataka (BoT), huduma za kifedha zimfikie kila mmoja na tunataka kwenda mbali zaidi kwa kuishauri Serikali kuweka kwenye sera zake na kutambua kwamba kupata huduma za kifedha ni haki ya kila raia na tunataka kuona benki inafanya nini katika kutoa huduma.

“Hili pia linatusaidia hata zinapokuja benki kuomba leseni kwamba tunamuuliza, je, unaweza kufanya biashara au unataka kutengeneza faida tu. Kama huwezi hatukupi leseni, hakuna sababu ya benki kufanya biashara kwa lengo la kupata faida bali iwe sehemu ya kimbilio na kutoa huduma,” alisema.

Alisema huduma za mabenki zinapaswa kufika chini hasa kwenye maeneo ya utoaji huduma za fedha jambo ambalo BoT inazitaka sekta za fedha ziwe na fedha muda wote.

SARAFU MPYA

Akizungumzia hatua ya Kenya kuzindua sarafu mpya na kama Tanzania ina mpango wa kufanya hivyo, Profesa Luoga, alisema hakuna mpango wakufanya hivyo.

“Ni kweli wametoa sarafu mpya (Kenya) na karibuniwatatoa noti mpya, lakini kwetu sisi Tanzania tuna sarafu za kutosha natunataka ziwe nyingi ili zitumike zaidi kwa lengo la kuhakikisha noti yetu inaishi muda mrefu zaidi.

“Noti yetu Tanzania ina ubora kwa zaidi ya asilimia 100 na inatengenezwa kwa pamba na kwa ubora noti ya Tanzania ni bora zaidi, lakini ikienda kwa watani zangu kule Kibondo (Kigoma), inaporudi inakuwa imechakaa zaidi.

“Lakini ukipeleka koini itakaa zaidi kuliko noti. BoT inataka fedha inapomfikia mwananchi iwe safi na katika kuhakikisha hilo inaangalia ubora wa fedha zako,” alisema Gavana Luoga.

Alisema tayari Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshapitisha sheria ya Benki ya Afrika Mashariki na ifikapo mwaka 2024 nchi wanachama zitakuwa na sarafu yake.

“Ninaamini kwamba kupitishwa kwa sheria hii ambayo inataka hadi mwaka 2024 tutakuwa na Benki ya Afrika Mashariki na hizi sarafu za kila nchi mwanachama nahisi nyingi zitabaki makumbusho,” alisema.

MZUNGUKO WA FEDHA

Akitoa ufafanuzi kuhusu dhana iliyojengeka kwa jamii kuhusu kushuka kwa mauzo kwa wafanya biashara wadogo na wakubwa, alisema pamoja na halihiyo bado haijaathiri mzunguko wa fedha kwa jamii.

Alisema pindi yanapotokea mabadiliko kwa kipindi fulani unaweza kusema huna fedha, lakini ukweli ni kwamba unapoona fedha hakuna maanayake fedha inaongezeka thamani.

“Kuna wakati Dar es Salaam watu walikuwa wanajenga majengo kwa haraka zaidi lakini hakukuwa na ujenzi wa viwanda. Hiyo maana yake fedha ilikuwa inatoka zaidi serikalini. Hapo zamani mtu alikuwa mpambaji tulakini fedha ambayo alikuwa anapata ni nyingi kiasi ambacho anaweza kujenga hekalu.

“Tafsiri yake ni kwamba, fedha nyingi za Serikali zilikuwa zinapigwa kwa mtu kulipwa kiasi kikubwa na kuona kwamba hakuna kama yeye. Sasa jiulize ilikuwa viwanda ni vile vile haviongezeki lakini watu walikuwa wanapata fedha nyingi.

“Si hilo tu hata wengine walikuwa wafanyakazi hatamshahara hawagusi kila kukicha ni mikutano na makongamano tena wakilipana fedha nyingi. Hali hiyo ndiyo iliwafanya wengine hata kukodi nyumba kwa dola 1,000 kwa mwezi kwa sababu anakusanya fedha nyingine zisizostahili lakini sasa hali imedhibitiwa,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles