Amina Omari, Tanga
Serikali imesema haitatoa usimamizi wa miradi ya maji kwa wakandarasi badala yake itazitumia mamlaka zake za maji ili kuhatakisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, wakati akipokea taarifa za sekta ya maji kuitoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela wakati wa ziara yake mkoani hapo.
Amesema kufanya hivyo kutasaidia kuzijengea uwezo mamlaka hizo katika utekelezaji wa miradi pamoja na kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tanga aliiomba serikali kuwasaidia kutafuta ufumbuzi wa kero ya huduma ya maji katika wilaya za Muheza, Pangani na Mkinga.