23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yafyeka Bajeti ya Bunge

Philip MpangoNA KHAMIS MKOTYA, DODOMA

SERIKALI imefyeka Sh bilioni 74 katika Bajeti ya Ofisi ya Bunge ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Kufyeka kwa fedha hizo kulitangazwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali bungeni kama moja ya mwendelezo wa mpango wake wa kubana matumizi.

Dk. Mpango alisema katika bajeti hiyo, fungu 42 mfuko wa Bunge umetengewa Sh bilioni 99.066, kati ya hizo Sh bilioni saba ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na Sh bilioni 23.798 kwa ajili ya mishahara.

Fedha hizo ni pungufu ya Sh bilioni 74 ikilinganishwa na zilizoidhinishwa katika bajeti ya mwaka 2015/2016, ambapo Mfuko wa Bunge ulitengewa Sh bilioni 173.768.

Dk. Mpango alisema mabadiliko ya Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, yamempa mamlaka waziri mwenye dhamana ya fedha kuwasilisha bungeni mambo ya fedha za matumizi ya mifuko miwili ya Bunge na Mahakama.

“Pamoja na kuwasilisha mbele ya Bunge mambo ya fedha, mafungu tisa niliyotaja, nichukue fursa hii pia kuwasilisha mambo ya fedha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 kwa mfuko wa Mahakama, fungu la 40 na mfuko wa Bunge fungu la 42.

“Maombi haya ni kwa mujibu wa marekebisho yaliyofanyika katika kifungu cha 59 kifungu kidogo cha tatu cha Sheria ya Utawala wa Mahakama na kifungu cha 29 kifungu kidogo cha tatu cha Sheria ya Utawala wa Bunge sura 115 kupitia Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015,” alisema.

Katika bajeti hiyo, fungu 40 la mfuko wa Mahakama umetengewa Sh bilioni 131.627, kati ya hizo Sh bilioni 48.297 ni kwa ajili ya mishahara, Sh bilioni 36.567 kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh bilioni 46.761 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akizungumzia nakisi hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Josephat Kandege, alisema punguzo hilo la bajeti ni mpango wa Serikali wa kubana matumizi katika idara na taasisi zote za umma.

“Kuna watu wanasema fedha zimepunguzwa kwa sababu ya chenji ya shilingi bilioni sita za Bunge zilizorudi Hazina, zile zilirudi si kwa sababu zilikosa shughuli za kufanyia hapana.

“Mwaka jana tulikuwa katika uchaguzi hapakuwa na Bunge, Oktoba hapakuwa na wabunge waliosafiri nje kwa sababu Bunge lilikuwa limevunjwa ndiyo maana fedha zile zilibaki,” alisema Kandege.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles