29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yabanwa dhana ya uvunaji maji

MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi, Asaa Othamn Hamad (CUF), ameitaka Serikali kueleza dhana ya uvunaji wa maji ya mvua imeishia wapi.
Akiuliza swali bungeni jana, Mbunge huyo alisema kutokana na mabadiliko ya tabianchi, licha ya kujaliwa rasilimali kama misitu, mito na maziwa, bado kuna maeneo yanayorejesha nyuma shughuli za kilimo.
“Je ile dhana ya Serikali ya kuvuna maji ya mvua, imeishi wapi?” alihoji.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage, alisema kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi na rasilimali za ardhi na maji zilizopo nchini, Serikali inachukua hatua za kutumia rasilimali hizo kwa kuhimiza kilimo hifadhi, kufanya utafiti za mazao na kuhimiza kulima mazao yanayokomaa haraka.
“Katika utekelezaji wa mipango ya kilimo cha umwagiliaji nchini, Serikali inaendelea kuboresha kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya skimu za umwagiliaji pamoja na ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua,” alisema.
Alisema Serikali imepanga kuendeleza kilimo cha umwagiliaji hadi kufikia hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2020 na hekta 1,500,000 ifikapo mwaka 2025.
Mwijage alisema pia Serikali itaendelea kuboresha na kuendeleza miradi ya umwagiliaji ya wakulima wadogo na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.
“Kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabia nchi, Serikali inaendelea kuhimiza uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa pamoja na kuendeleza teknolojia za umwagiliaji zenye ufanisi katika matumizi ya maji kama umwagiliaji wa matone,” alisema Mwijage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles