23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Fedha za barabara ya Turiani, Mikumi zasakwa

SERIKALI imesema bado inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Turiani hadi Mikumi, katika sehemu ya Ulaya hadi Mikumi yenye urefu wa kilomita 43.7.
Akijibu swali bungeni jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge, alisema ujenzi wa barabara ya Turiani hadi Mikumi umegawanywa katika awamu nne.
Alisema sehemu ya kwanza ni kutoka sehemu ya Magole hadi Turiani, yenye urefu wa kilomita 45 ambapo sehemu hiyo imeshakamilika kwa asilimia 69.
“Sehemu ya pili ni kutoka Dumila hadi Rudewa yenye urefu wa kilomita 45, ujenzi wa sehemu hii umekamilika, sehemu ya tatu ni kutoka Rudewa hadi Ulaya yenye urefu wa kilomita 53.3, ujenzi wa sehemu hii kwa kiwango cha lami utaanza katika mwaka wa fedha 2015/16,” alisema.
Lwenge alisema sehemu ya nne ya kipande cha kutoka Ulaya hadi Mikumi chenye urefu wa kilomita 43.7, usanifu wa sehemu hiyo umeshakamilika.
Alisema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu hiyo kwa kiwango cha lami.
Lwenge alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Christine Ishengoma (CCM), aliyetaka kujua lini ujenzi wa barabara ya Turiani hadi Mikumi kwa kiwango cha lami utakamilika na sababu za kusimama kwa mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles