27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali yaanzisha kurugenzi ya wakunga

pindaNa Shomari Binda, Musoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imeanzisha Kurugenzi ya Wauguzi na Wakunga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili kwenye utoaji wa huduma kwa umma.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na wauguzi na wakunga pamoja na wakazi wa Mkoa wa Mara kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mukendo mjini Musoma.
“Nina taarifa kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha 2015/2016, kurugenzi hiyo itakuwa na bajeti yake yenyewe itakayotumika kuboresha huduma za wauguzi na wakunga nchini. Haya yote yanafanyika kwa kuwa Serikali inatambua na kuthamini shughuli za wauguzi na wakunga hapa nchini,” alisema.
Alisema mafanikio yaliyofikiwa ya kupunguza vifo vya watoto na wanawake yamechangiwa na kazi nzuri zinazofanywa na wakunga licha ya kuwa kada hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi.
Pinda alisema ili kukidhi mahitaji ya wakunga nchini, Serikali imeongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na fani ya uuguzi na ukunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles