32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaahidi kuendelea kurejesha miundombinu iliyohalibiwa na mvua Dar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amepongeza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada mbalimbali za kurejesha hali katika maeneo ambayo miundo mbinu ya barabara imeathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake leo Januari 21,2024 mkoani humo alipotemebelea na kujionea athari za mvua zilizoonyesha usiku wa kuamkia Januari 20, mwaka huu na kuathiri maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ubungo, Kindondoni, Temeke, Kigamboni na Jiji la Ilala.

Katika picha ni baadhi ya maungio ya madaraja ambayo yameathrirka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na juhudi kubwa zikifanywa na serikali usiku na mchana katika kurejesha mawasiliano ya barabara katika maeneo ya maungio ya madaraja hayo ili yaendelee kupitika.

Naibu Waziri Ummy alisema anampongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abert Chalamila kwa uongozi ambao wameuonesha katika kurejesha hali na kazi waliyofanya.

“Naomba tufanye kazi hii usiku na mchana ili tuweze kurejesha hali mapema bila kuathiri shughuli za biashara na shughuli nyingine za uchumi zinazofanyika katika Mkoa wa Dar es Saalam.

“Sisi kama serikali tunawahakikishia wana Dar es Salaam kwamba tutafanya kazi hii ya urejeshaji wa hali kwa nguvu bila kuchoka,” amesemaUmmy.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Saad Mtambule amesema kazi waliyofanya ni kusimamia usafishaji wa mitaro na usawishaji wa mito na hivyo kusaidia maji kutotuwama kwa muda mrefu.

“Tumeendelea kuwaeleza wananchi walio katika maeneo ya pembezoni mwa mito kama; mto Nyakasangwa, mto Mpiji, mto Tegeta, mto Mlalakuwa na mto Ng’ombe kuhamia maeneo ya juu ili kuepuka athari za mvua,” amesema Mtambul.

Amesisitiza kuwa ujenzi wa nyumba holela umesababisha watu kujenga mpaka kwenye mapito asili ya maji na kusababisha maji kukosa sehemu za kupita na kuingia maeneo ya watu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga akiwa amembeba mtoto wakati alipotembelea kuona urejeshaji wa maungio ya daraja katika ya barabara ya Tanganyika katika daraja la Mbweni yaliyoathiriwa kutokana na Mvua za vuli zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

“Lakini pia tuna kazi ya kuendelea kuwaelimisha wananchi ili wafuate misingi ya ujenzi wa maeneo kulingana na ramani ya mipango miji,” alisisitiza.

Akizungumza katika ziara hiyomk azi wa Ununio, James Koyi ameishukuru serikali kwa kazi kubwa inayofanya ya urejeshaji wa hali katika maeneo yaliyoathirika mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles