24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali: Vyama vya Wafanyakazi havitaingiliwa

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesema itaendeea kuwezesha uwepo wa majukwaa ya wafanyakazi ili kuhakikisha yanatoa nafasi ya wafanyakazi kujadili masuala yao.

Hayo yamebainishwa Mei 17, na Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri chini, Pendo Berege, katika mafunzo kwa watendaji wa vyama vya wafanyakazi, waajiri na shirikisho la vyama hivyo yaliyofanyika mkoani Morogoro yakilenga kukumbushana wajibu na majukumu katika utekelezaji wa katiba na kanuni za vyama.

Amesema ataendelea kushirikiana na vyama vya wafanyakazi ili kuhakikisha vyama hivyo vinatekeleza majukumu kwa weledi na bila kuingiliwa na kuwa majukwaa ya kujadili mambo yao.

Amesema katika sherehe za Mei Mosi Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ilielekeza vyama vya wafanyakazi kuhakikisha vinawasilisha masuala ya wafanyakazi serikalini hivyo majukwaa hayo ni kiunganishia ycha kushughulikia maslahi ya wafanyakazi.

“Nimshukuru sana Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye serikali anayoiongoza imeendelea kutoa kipaumbele kwa wafanyakazi nchini na kuhakikisha kwamba vyama vya wafanyakazi vinaendelea kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa na kwa weledi mkubwa na mwisho viweze kuwaunganisha wafanyakazi wengi nchini na vyama vya waajiri viweze kuwaunganisha waajiri wengi nchini ili tupate daraja na majukwaa yanayogusa uchumi wa nchi kwani hao ndiyo wanagusa uchumi wa nchi hii.

“Hivyo, ni imani yangu kwamba kutokana na mafunzo mliyoyapata hapa ni bayana kwamba mmepata majibu ya maswali yenu kwani mafunzo mliyopata ni mazuri na yatasaidia kutekeleza majukumu yenu kwa weledi zaidi.

“Milango iko wazi muda wowote na niwatake tu kwamba muendelee kushirikiana na ofisi ya Msajili kwani ndiyo nyumbani kwenu,” amesema Barege.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya ametoa rai kwa Msajili wa vyama hivyo kuwasilisha ombi la ada ya uwakala serikalini isiingiliwe na watu serikalini ili kuondoa changamoto zinazojitokeza.

Awali, Mwakilishi wa Chama Cha Waajiri (ATE), Leonard Mapha, ameshauri kuendelea kuwepo kwa mijadala yenye manufaa na kuwa na mikataba bora mahali pa kazi ili kuweka wazi matarajio yao baina ya mwajiri na mwajiriwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles