27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kutumia mfumo wa M Kilimo kukabiliana na uhaba wa maofisa ugani

Safina Sarwatt,Moshi

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeanza mpango wa kukabiliana na uhaba wa Maofisa ugani hapa nchini kwa kutumia mfumo wa M Kilimo kupitia teknolojia ya simu za mkononi kutoa elimu kwa wakulima zaidi milioni tano ambao tayari wamesajili kwa mfumo huo.

Mtaalamu wa ugani wizara ya kilimo, Zacharia Gadiye ameyasema hayo jana wakati wa Maadhimisho ya wiki ya chakula duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro.

Amesema lengo la mfumo huo ambao umezinduliwa mwaka jana ni kuhakikisha wanawafikia wakulima na wafugaji zaidi ya milioni saba hapa nchini.

Amesema mfumo huo unawezesha wakulima kupata elimu kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi baada ya kusajili na hatimaye kupata taarifa za ugani ambazo wanahitaji kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Amesema kwa sasa nchi inakabiliwa na uhaba wa maafisa ugani zaidi ya elfu kumi na tatu na kwamba maafisa ugani waliopo kwa sasa ni elfu sita mia saba na nne(6704) ambao hawatoshelezi.

Amesema kwa sasa changamoto kubwa kwa maafisa ugani waliopo ni ukosefu wa simu janja za mkononi ambazo zinawawezesha kujiunga na mfumo huo,kwa kusaidia wakulima na wafugaji.

“Pamoja na maafisa ugani waliopo kwa sasa kutokuwa na simu janja ambazo zinawawezesha kupata taarifa kwa wakati jambo ambalo tayari serikali imeanza kulifanyia kazi,”amesema.

Amesema mfumo huo pia utawezesha wakulima kupata masoko ya bidhaa wanazozalisha kwa urahisi na hivyo kupunguza gharama utafutaji wa masoko

Amesema wakulima wanachotakiwa kufanya ni kujiunga na mfumo huo kupitia simu za mkononi za Aina zote kwa kupiga namba 15200# ili kujisajili tayari kwa kupata huduma zote za ugani wanazohutaji.

Hata hivyo ofisa huyo amesema bado wanaendelea na programu ya kutoa elimu kwa wakulima nchi nzima hivyo akatoa kwa wananchi na wafanyabiashara nchini kujiunga na mfumo wa M.Kilimo kupata taarifa za masoko na mbinu Bora za uzalishaji wa mifugo na Kilimo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles