27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania 940,507, wamepata chanjo ya Uviko 19

Na Clara Matimo, Mwanza

Watanzania 940,507, wamepata chanjo ya Uviko 19 sawa na asilimia 88.9 ya chanjo zote 1,058,400 aina ya JJ zilizoingia nchini awali huku lengo la serikali likiwa ni kutoa chanjo kwa asilimia 60 ya wananchi wote.

Hayo yamebainishwa jijini Mwanza Oktoba 17, 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa,  wakati akitoa taarifa ya serikali ya  wiki  kwa waandishi wa habari mkoani humo.

Amesema shehena ya chanjo 1,065,000 aina ya Sinopharm zilizoingia nchini wiki iliyopita kutoka nchini China zimeanza  kusambazwa katika halmashauri na mikoa yote ambapo zoezi la kuchanja wananchi linaendelea.

“Pamoja na chanjo hizo pia tunatarajia kupokea chanjo zingine aina ya Pfizer dozi 500,000 mwishoni mwa mwezi huu wa kumi kutoka Covax Facility ambazo ni sehemu ya dozi milioni 3.7 za chanjo aina ya pfizer ambazo nchi yetu itazipata kwa awamu,”amesema na kuongeza:

“Hivi ninavyoongea majokofu ya baridi kali 14 yenye uwezo wa kuhifadhi chanjo milioni 3.7 yameishafungwa pale jijini Dar es Salaam lakini kupitia Covax Facility tunatarajia kupata dozi milioni 11.8,”amesema Msigwa.

Aidha Msemaji huyo  wa serikali amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona kama wanavyoelekezwa na madaktari ikiwemo kuchanjwa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa, kuepuka misongamano, kufanya mazoezi na kula vyakula vyenye  lishe  bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles