30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kushirikisha wananchi kuondolewa kwa kijiji cha Mgaresero pori la Pololet

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imesema kuwa itashirikisha wananchi kuhusu utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri ya kukiondoa Kijiji cha Ngaresero katika Pori Tengefu la Ziwa Natron kutokana na sababu kwamba Pori hilo ni moja kati ya maeneo yaliyotolewa maelekezo na Baraza la Mawaziri kuwa lipandishwe hadhi.

Hayo yamesemwa leo Mei 16, 2023 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Lekishon Shangai, lililoulizwa na Zaytun Swai kuhusu lini Serikali itaondoa Kijiji cha Ngaresero kwenye eneo la Pori Tengefu la Pololet baada ya kujumuishwa kimakosa.

Amefafanua kuwa kulingana na Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2019, ardhi ya Pori Tengefu Ziwa Natron ipo kwenye kundi la ardhi ya Hifadhi.

Aidha, Masanja ameweka bayana kuwa Serikali itaenda kushughulikia mgogoro huo kwa kukutana na wananchi ili kufikia muafaka na hatimaye pori hilo liwe na hadhi iliyotarajiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles