27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Silent Ocean yarahisisha biashara Tanzania na India

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya kusafirisha mizigo ya Silent Ocean imezindua tawi jipya chini India Mombahai kwa ajili ya kutatua changamoto ya wafanyabiasha kusafirisha mizigo nchini humo

Akizungumza leo Dar es Salaam Mei 16, wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Silent Ocean, Mohammed Soloka wakati wa uzinduzi huo amesema wamefungua tawi hilo kutokana na fursa nyingi zilizoko India.

“India ni nchi ya pili duniani inayokua kwa kasi katika biashara na tuliona changamoto ya kuchelewesha kwa mizigo kufika nchini tukaamua kufungua tawi hilo na tumefanya hivyo kwa ajili ya kukuza wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa,” amesema Soloka.

Amesema siku zote wapo na wafanyabiashara nakwamba hiyo ni fursa kwa Serikali kukusanya mapato na kukuza uchumi wa nchi kupitia tawi hilo na wafanyabishara watasafirisha mzigo kutoka India hadi Tanzania kwa siku 17 hadi 25 kwa muda mfupi.

Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo, Abdalah Mwinyi amesema wanahaki ya kuwapongeza Silent Ocean kutokana na kurahisisha kufika kwa wakati mizigo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Tuna kila sababu ya kuishukuru kampuni hii kwani kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita mizigo kufika nchini ilichuku muda wa miezi mitatu hadi sita.

“Siku hizi mbili tunapitia kwenye wakati mgumu tunaimani kikao cha kesho na Waziri Mkuu kitaleta matunda, tunashukuru Silent Ocean kwa kuongeza tawi lingine,” amesema Mwinyi.

Nae Mwakilishi wa Wafanyabishara, Wahid Abdulghafoor amesema wafanyabishara wa nchi hizi mbili walikuwa na changamoto ya usafirishaji wa mizigo hivyo kwa sasa wanahitaji kufanya kazi na Silent Ocean.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles