30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kurejesha Mawasiliano ya barabara iliyokatika

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mbunge wa Ileje na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewahakikishia wananchi wa Kata ya Sange na Ngulugulu kuwa Serikali itahakikisha inarejesha mawasiliano ya miundombinu ya barabara iliyokatika.

Mhandisi Kasekenya amaeyasema hayo April 30, 2022 baada ya kutembelea maeneo ambayo yameathiriwa na mvua ambazo zinaendelea kunyesha wilayani humo, ambazo hivi karibuni zimesababisha watu watano kufariki dunia baada ya nyumba zao kuangukiwa na kifusi.

Amesema tayari Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) mkoani humo pamoja na wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wilayani humo kwa kushirikiana na wananchi wamewnza jitihada za kuondoa kifusi kilichopo barabarani huku wakisubiri vifaa vya kama greda na katapila kwa ajili ya shughuli hiyo.

“Wakati tunasubiri greda na katapila wananchi wameona shughuli zao kiuchumi zitakwama wakaona ni bora wajitolee ili kurahisisha mawasilinao ambayo yamekwama huku wakihofia usalama wa watoto wao kwenda shule na hili wamelifanya kwa asilimia 100.

“Wazazi na walezi hakikisheni mnakuwa waangalizi kwa watoto wenu hasa katika kipindi hiki ambacho kwa ukanda wa tarafa ya Bundali kwa mvua zinazoendelea kunyesha magema ya milima inameguka na kuhatarisha maisha yao,” amesema Mhandisi Kasekenya.

Upande wake, Martin Msokwa mwananchi wa Kijiji cha Sange amesema baada ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara wameanza kujitolea kutoa kifusi kwa kutumia majembe ya mkono na kuiomba serikali kipeleka makatapira kwa ajili ya kurahisisha kazi ya kutoa kifusi.

“Sisi wananchi tumejitolea kuondoa kifusi lengo likiwa ni kufungua barabara kwani tunashindwa kusafirisha mizigo kwenda mnada wa Katengele hivyo serikali kupitia TANROAD Songwe,” amesema Msokwa.

Mkazi wa Kijiji cha Ngulugulu, Ngupilikwa Kabuje amesema kukatika kwa mawasiliano ya barabara kwa kuzibwa na magema yaliyoporomoka wapo hatarini kutopata huduma za kijamii ikiwepo wamama wajawazito kuwa hatarini kwani hakuna aina yoyote ya usafiri inayoweza kuwafikisha vituo vya kutolea huduma za afya.

“Tumeanza kutembea kwa mguu umbali mrefu baada ya barabara kuangukiwa na magema ya udongo wa kifusi kufuata huduma soko la Katengele umbali wa zaidi ya Km 20 kwani usafiri umekuwa ni shida Kila mtu akihifiwa kuangukiwa na kifusi” amesema Kabuje.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mvua zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo wilayani Ileje zilisababisha maafa ambapo watu watano walifariki dunia akiwepo mama mjamzito wa miezi tisa pamoja na ng’ombe wanne sambamba na miundombinu ya barabara inayosimamiwa na TANROAD na TARURA zilikata mawasiliano hali inayopelekea wananchi kukosa baadhi ya huduma kama masomo kwa wanafunzi huku wazazi wakihofia watoto kuangukiwa na kifusi.2. PICHA YA WANANCHI WAKIONDOA KIFUSI KATIKA KIJIJI CHA SANGE3.PICHA YA MBUNGE AKIKAGUA ENEO LILIPOFUNGA BARABARA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles