26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kukusanya fedha za waathirika wa ajali ya MV Nyerere

Na Mwandishi Wetu- Ukerewe


SERIKALI imesema itafungua akaunti maalumu kwa ajili ya kukusanya fedha zitakazowasaidia waathirika wa ajali ya Kivuko cha MV Nyerere.

Akizungumza jana katika Kisiwa cha Ukara baada ya kupokea msaada wa Sh milioni 10 kutoka katika Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, alisema akaunti hiyo itafunguliwa kupitia ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Alisema akaunti itafunguliwa chini ya sheria ya maafa inayoelekeza kuwa yanapotokea maafa mkoa husika unapaswa kufungua akaunti itakayotumika kukusanya fedha kusaidia waathirika.

Alisema fedha zitakazochangishwa zitatumika kuwasaidia waathirika wa ajali hiyo na si vinginevyo.

UFAFANUZI SIKU ZA MAOMBOLEZO 

Katika hatua nyingine, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais-Ikulu jana ilitoa  ufafanuzi kuhusu siku nne za maombolezo  zilizotolewa juzi na Rais Dk. John Magufuli, baada ya kuwapo kwa sintofahamu kwa baadhi ya watu waliodhani kesho kutakuwa ni mapumziko.

Ufafanuzi huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, kupitia ukurasa wake wa Twitter na kueleza kuwa kesho Jumatatu itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida na si mapumziko.

“Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu (kesho) Septemba 24, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya kitaifa itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida, Rais (Dk. Magufuli) ametangaza siku nne za maombolezo na si mapumziko,” aliandika Msigwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles