30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 12, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali kuendelea kutoa mafunzo ya cheti cha sheria

SERIKALI imesema itaendelea kutoa mafunzo ya ngazi ya cheti na stashahada katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuwa bado inawahitaji wataalamu hao.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi).

Katika swali lake, Machali, alihoji uhalali wa Serikali kupoteza fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo ya cheti na stashahada katika chuo hicho wakati haiajiri tena mahakimu wa ngazi ya cheti na stashahada.

Mwalimu alisema Serikali bado inawahitaji wataalamu hao ambao inawaajiri kama makarani wa mahakama na washauri wa sheria katika taasisi mbalimbali za Serikali.

“Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto bado kinatoa mafunzo ya cheti na stashahada na katika mwaka huu wa fedha tutadahili zaidi ya wanafunzi 1,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles