28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Nyamagana waanza kufanyiana ushushushu

Na John Maduhu, Mwanza
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, kimeunda kamati za siri ili kufuatilia mienendo ya wagombea waliotangaza nia ya kuwania Jimbo la Nyamagana.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana, Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Elias Mpanda, alisema lengo la kuunda kamati za siri ni kudhibiti wagombea wanaotoa rushwa kwa wanachama wa CCM ili kuwashawishi kuwaunga mkono.

Alisema kamati hizo za siri pia zitakuwa na jukumu la kufuatilia kama watangaza nia hao wamekuwa wakichafuana wao kwa wao wanapokutana na wanachama katika kata mbalimbali kwa ajili ya kujitambulisha.

Alisema kamati hizo za siri zinakusanya taarifa za kila siku za wagombea waliotangaza nia ya kugombea Nyamagana ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ezekiel Wenje.

“Kabla ya kuunda kamati hizo za siri tulilazimika kuwaita watangaza nia wote na kukaa nao katika sekretarieti ya chama wilaya, tuliwaeleza kuwa ni marufuku kutumia rushwa ili kusaka uungwaji mkono, pia tuliwaeleza ni marufuku kuchafuana wanapokutana na wanachama.

“Tulibaini kuwa tulipoteza kiti cha ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kutokana na wagombea kuchafuana na kujengeana chuki, hatukuwa wamoja ndiyo maana tulipoteza, tuko makini na wagombea wasije kutulaumu kwa vitendo vyao,” alisema Mpanda.

Alisema hawatakuwa na simile na mgombea atakayebainika kwenda kinyume na maelekezo, kanuni na katiba ya chama kwa sababu atafutiwa nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles