24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji

Na Clara Matimo, Mwanza

Serikali imesema inaendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji katika ngazi zote za elimu kuanzia Msingi, Sekondari, Vyuo vya kati na Elimu ya juu ili kuleta tija kwa wahitimu wawapo katika soko la ajira.

Hayo yanmebainishwa leo Aprili 25, 2023 jijini hapa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na wadau wa elimu kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la Maktaba na Maabara za Sayansi na Tehama katika Chuo cha Ualimu Butimba kilichopo wilya ya Nyamagana mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Prof. Mkenda amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pia inaendelea kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo kuandaa walimu watakaokidhi soko la ajira wanaosoma katika vyuo vyote 35 vya ualimu vilivyopo nchini.

“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kwamba wanafunzi wakihitimu waweze kujiajiri, dhamira yake na anachotaka ni elimu yetu hapa nchini iongeze ujuzi kwa vitendo,” amesema Prof.Mkenda.

Akizungumzia miaka 59 ya Muungno wa Tanganyika na Zanzibar itakayoadhimishwa kesho April 26 2023, Prof. Mkenda amewaasa vijana wanaosoma vyuoni wasimamie muungano huo bila kuyumba, kutetereka na kubabaika ili kuwaenzi waasisi wa nchi hii na kudumisha amani iliyopo.

“Chuo hiki kimeanza mwaka 1939 hadi leo vijana kutoka sehemu balimbali nchini wanakuja hapa kusoma hii ni kutokana na amani na utulivu iliyopo katika nchi yetu ambayo ni matunda ya waasisi wa nchi hii hivyo tusimame kidete kuutetea na kuulinda kwa kila hali muungano wetu,” amesema Prof. Mkenda.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amesema kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 na 2021/2022 Serikali ya awamu ya sita imeimarisha Elimu ya Ualimu kwa kupeleka fedha katika vyuo vya Ualimu kwa ajili ya mafunzo ya walimu tarajali na mafunzo kazini kwa watumishi ambapo Chuo cha Ualimu Butimba kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 na 2021/2022 kilipokea zaidi ya Sh bilioni moja kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara za Fizikia, Kemia Maabara ya Tehama, Vyumba vinne vya madarasa, Ukumbi wa mihadhara na kukarabati majengo ya Maabara ya Baiolojia na Maktaba.

“Pia katika kipindi cha mwaka 2021/2022 na 2022/2023 Serikali ya awamu ya sita ilileta fedha katika chuo hiki cha Ualimu Butimba kiasi cha Sh milioni 715,163,287.28 kwa ajili ya kugharamia Mafunzo ya Ualimu kwa vitendo, mafunzo hayo hutoa fursa kwa wanachuo kupata tajiriba ya kumudu Maisha ya kazi na uhalisia wa Mazingira ya kazi,” ameeleza Malima.

Akisoma taarifa ya mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Maabara za Sayansi, Tehama na Maktaba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof.Carolyne Nombo, Mkurugenzi Msaidizi Ualimu wa Wizara hiyo, Huruma Mageni amesema mradi huo umetekelezwa kupitia mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) kwa gharama ya Sh milioni 467,695,598.00.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles