30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuboresha mawasiliano mwambao wa Ziwa Viktoria

Na Yohana Paul, Geita

SERIKALI imepanga kuboresha mtandao wa mawasiliano ndani ya ziwa victoria ili kuimarisha usalama wa wavuvi na wasafiri na kuwasaidia kupata msaada wa haraka pindi wanapokutana na dhoruba yeyote.

Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Huduma za Meli Tanzania (TASAC) mkoa wa Geita, Rashid Katonga ameeleza hayo alipokuwa akizungumuza na wavuvi wa mwalo wa Kalilutale wilayani Chato.

Katonga amebainisha Tasac itaambatanisha mpango huo na ujenzi wa vituo vya utafutaji na uokoaji ndani ya ziwa na utatekelezwa kwa ushirikiano na usimamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amesema hatua hiyo inakuja kwani changamoto ya mawasiliano katika mwambao wa ziwa Viktoria na maeneo ya jirani ya nchi kavu si tu inawathiri wavuvi bali pia inakwamisha ufanisi wa shughuli za Tasac.

“Shughuli nyingi tunazozifanya Tasac, za usajili, uandaaji wa bili za malipo zinategemea mifumo ambayo inahitaji kuwepo kwa mtandao, kwa hiyo mtandao usipokuwepo huwezi kufanya chochote,” amesema.

Amesema uwepo wa mtandao ndani ya ziwa Viktoria utaimarisha mawasiliano ya simu na vyombo vya usafiri na kuiwezesha Tasac kutekeleza jukumu la utafutaji na uokoaji kwa urahisi ajali inapotokea.

Amefafanua mpango umeanza kwanza kwa kung’amua maeneo yenye changamoto, pili kupeleka taarifa kwenye mamlaka husika ambao ni TCRA na kisha kuwapitisha kwenye maeneo yenye uhitaji.

Awali mmiliki wa vyombo vya uvuvi mwalo wa Kalilutale, Ndange Kiberenge amelalamikia changamoto ya mtandao ndani ya ziwa inahatarisha usalama wa wavuvi hususani inapotokea ajali ama wanapotekwa.

Naye Mvuvi katika Mwalo wa Kalilutale, Zagalo Keberenge amesema mawasiliano yakiboreshwa yatasaidia viongozi waliopo mwaloni kuwasiliana kwa urahisi na wavuvi waliopo ndani ya ziwa wakati wa dharura.

Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Geita, Tito Mlewa amewahakikishia wavuvi serikali ya awamu ya sita itahakikisha inamaliza changamoto walizonazo ili kuimarisha sekta ya uvuvi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles