25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Betika wahitaji mabingwa 100 msimu wa 5 wa Kibingwa

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya mchezo wa kubashiri Betika imesema katika msimu wa tano wa mtoko kibingwa wanahitaji mabingwa 100watakaoshuhudia mtanange wa Simba dhidi ya Yanga utaopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Aprili 16, mwaka huu.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Februari 20, 2023 jijini Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa Betika, Juvenaous Rugambwa amesema mtoko wa kibingwa msimu wa tanowamepata mabingwa kutoka mikoa mbalimbali huku wakiwa bado watu 95 kukamilisha watu 100.

“Katika wiki ya kwanza ya promotion hii tulikua na droo tatu na droo hizo tumepata jumla ya mabingwa 5 ambao ni Mariamu kutokea Chamazi, Fahame kutokea Simiyu, Clement kutokea Songea, Steven kutokea Kagera na Joshua Charles kutoka Mkuranga, hivyo imebaki mabingwa 95 ambao watatokea mikoani na watapata tiketi za ndege kwenda na kurudi na watalala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota 5 wakiwa jijini Dar es Salaam,” amesema Rugambwa.

Ameongeza kuwa kushiriki kwenye droo beti mikeka 5 kila siku na kwa kila mkeka weka dau la kSh 500 na kuendelea ambapo mshiriki ataingia moja kwa moja katika droo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,407FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles