27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali imedhamiria kuwekeza katika elimu mtoto wa kike- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mradi wa shule maalumu ya sekondari ya wasichana Ruangwa na amesema kwamba Serikali imeadhamiria kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike kwa lengo la kumuwezesha kutimiza ndoto zake kielimu.

Baada ya kukagua mradi huo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na maendeleo yake na amewataka waliokabidhiwa jukumu la kusimamia ujenzi huo waendelee kuwa waaminifu na wahakikishe wanashirikiana vizuri na mjenzi ili akamilishe kwa wakati uliokusudiwa.

Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa mradi huo (Ijumaa, Februari 26, 2021). Shule hiyo ya mchepuo wa sayansi inayojengwa katika kijiji cha Dodoma kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa kupitia fedha za mpango wa lipa kwa matokeo (EP4R), ambapo awamu ya kwanza imegharimu sh. milioni 700.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kunatarajiwa kuinua kiwango cha ufaulu kwa mtoto wa kike ambaye ndiyo mlengwa.

”Tumedhamiria kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wa kike kwa kuwaboreshea mazingira ya kujifunzia. Tunataka watoto wa kike wasome bila usumbufu,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema walianzisha mradi wa ujenzi wa shule ya wasichana katika wilaya hiyo ili kutoa nafasi nzuri kwa mtoto wa kike kupata fursa ya kusoma vizuri akiwa katika mazingira rafiki yatakayo muepusha na changamoto mbalimbali zinazowafanya washindwe kutimiza ndoto zao kielimu

Awali, Waziri Mkuu alitembelea shule ya msingi Chikoko iliyoko katika kata ya Makanjiro ambapo amewataka wananchi washikamane na wajitokeze kwa wingi katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa madarasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles