26.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri Mabula haridhishwi na huduma za ardhi Njombe

Na Mun Shemweta, Njombe

Wakati Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha sekta ya ardhi inapiga hatua katika kupanga, kupima na kumilikisha ardhi, mkoa wa Njombe kupitia halmashauri zake umeonekana kuwa nyuma katika juhudi hizo na kumfanya Naibu Waziri wa Ardhi, Dk. Angeline Mabula, kutoridhishwa na utoaji huduma za sekta ya ardhi katika mkoa huo.

Hali hiyo imebainika wakati wa kikao cha kazi baina ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dk. Mabula na watendaji wa sekta ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Njombe kilichofanyika FFebruari 25, 2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Akisoma taarifa ya utekelezaji kazi za ofisi ya ardhi mkoa wa Njombe, Kmaishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Njombe, Christopher Mwamasage, amesema, tangu kuanzishwa ofisi ya ardhi Mkoa mwezi Machi, 2020 ofisi hiyo imetekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kuandaa michoro 59 ya Mipango Miji.

Hata hivyo, halmashauri za Makete na Ludewa katika taarifa yake zimeonesha kutofanya vizuri kwa kushindwa kuidhinisha hata mchoro mmoja.

Aidha, halmashauri za Makete, Ludewa na ile ya Njombe zimeshindwa pia kufanya lolote katika zoezi la urasimishaji makazi huku katika utekelezaji kazi za upimaji na ramani mkoa ukiwa umeidhinisha mashamba matatu pekee na halmashauri ya wilaya ya Njombe ikiidhinisha ramani na kiwanja kimoja na halmashauri Makete ikiwa haina mchoro wala kiwanja ilichoidhisha.

Katika zoezi la utoaji hati na makusanyo ya kodi ya pango la ardhi, Mwamasage alisema jumla ya hati 1,136 zilisainiwa na mkoa ulikusanya shilingi 774,346,269 kati ya Sh bilioni 5.3 ilizopangiwa kukusanya mwaka wa fedha 2020/2021 huku mkoa ukipeleka wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi 22 katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya wanaodaiwa Sh 294,930,957.

Mabula alionesha kutoridhishwa na huduma za sekta ya ardhi zinazotolewa katika mkoa wa Njombe na Kuzijia juu halmashauri za wilaya za Makete na Ludewa kwa nyuma sana katika kutekeleza majukumu ya sekta ya ardhi.

‘’Hakuna eneo linalohitaji urasimishaji, umilikishaji hata wa mashamba, hata hati za kimila hii inasikitisha sana na kwa staili hii hatuwezi kufika, yaani Makete sifuri hakuna chochote, kwa hali hii mnawasaidiaje wananchi?,’’ alisema Dk. Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, kwa mwenendo uliooneshwa na halmashauri za Makete na Ludewa haina maana ya kuwa na ofisi za ardhi za mkoa  na kusisitiza kuwa baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri wanaona hali hiyo ni sawa wakati wao ni mamlaka za upangaji katika maeneo yao.

Aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi kubadilika na kufanya kazi kwa weledi na kujitahidi kufanya vizuri katika utendaji kazi ambapo aliwaeleza kuwa kila Mkuu wa Idara ya Ardhi ama Afisa ardhi Mteule atapimwa kutokana na utendaji wake ikiwemo kiasi cha fedha alizokusanya katika kodi ya pango la ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles