24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serena Hotel yazushiwa kutolipa kodi

Dar-es-Salaam-Serena-HotelNA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM.

HOTELI ya kimataifa ya Serena jana ilikumbwa na msukosuko wa kuandamwa na waandishi wa habari baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa imefungwa kwa amri ya serikali kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

Tetesi hizo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana asubuhi, zikieleza kuwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wameifunga hoteli kufunga kwa kukwepa kuliko kodi serikalini.

Mbali ya kusambazwa kwa uvumi huo, zilitumwa pia picha zilizokuwa zikionyesha sehemu ya hoteli hiyo ikiwa imezungushwa uzio uliokuwa na rangi nyeupe na nyekundu ambao ni alama inayotumika kuonyesha kusitisha kwa huduma katika eneo hilo.

Tetesi hizo zilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa uongozi wa hoteli hiyo ulikuwa mbioni kubadilisha jina kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.

Hata hivyo, MTANZANIA Jumamosi baada ya kufika hotelini hapo kwa lengo la kufuatilia ukweli wa tetesi hizo lilikuta shughuli za ukarabati wa sehemu ya kupokea wageni zikiendelea, huku wageni wakielekezwa kutumia mlango wa dharura ambako kumetengezwa sehemu ya muda ya kupokelea wageni.

Uongozi wa Hoteli ya Serena kupitia Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko, Seraphine Lusala, ulilazimika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ukikanusha kufungwa kwa hoteli hiyo na kusisitiza kuwa kinachoendelea hotelini hapo ni matengenezo.

“Si kweli kama hoteli imefungwa, tunafanya matengenezo na yalikuwa yafanyike tangu miaka mitatu iliyopita, kilichofanyika sasa ni kubadilisha eneo la mapokezi yaliyohamishiwa milango mingine na tumeanza na eneo hilo pamoja na sehemu ya mazoezi,” alisema Lusala.

Alisema matengenezo hayo yanalenga kuifanya hoteli hiyo kuwa ya kiwango cha juu zaidi na yatachukua miezi ya 10.

Lusala alisema awamu ya kwanza ya matengenezo itachukua miezi minne na miezi minne ijayo itahusu matengenezo sehemu ya vinywaji, chakula, eneo la uwanja na baadaye maeneo mengine ya wazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles