27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Sera ya elimu bure inavyowatesa Wakenya-2

Wanafunzi nchini KenyaMICHAEL MAURUS NA MITANDAO

KENYA imekuwa ikitajwa kuwa miongoni mwa nchi za Afrika zinazotoa elimu bora, japo wapo wanaopinga hilo, wakiwamo baadhi ya Watanzania.

Wanaoisifia Kenya kielimu, wanadai kuwa Wakenya wamekuwa na uelewa wa hali ya juu katika mambo mbalimbali kutokana na msingi uliojengwa katika elimu yao kuanzia ya awali hadi vyuoni.

Kwa wale wanaopinga hilo, wamekuwa wakidai kuwa kinachowabeba Wakenya dhidi ya raia wa nchi nyingine za Afrika Mashariki, ni uwezo wao mkubwa wa kuzungumza Kiingereza na si uelewa wa mambo kulingana na elimu yao.

Uwezo mkubwa wa Wakenya katika kuzungumza Kiingereza, umetokana na mfumo wao wa elimu ambapo kuanzia ngazi ya awali, masomo hufundishwa kwa lugha hiyo, hali inayomfanya mtoto anapofikia umri wa kuanza shule ya msingi, kuwa fundi wa kuzungumza lugha hiyo.

Lakini pia, wapo wanaodai kuwa Wakenya si kwamba ni watu walioelimika zaidi ya wengine ndani ya ukanda huu, bali kinachowabeba ni ujanja wao wa kuchangamkia fursa mbalimbali, lakini pia ‘uchapu’ wao unaobebwa na uchapakazi wawapo sehemu ya kazi.

Ijumaa ya wiki ya juzi, tuliona mfumo mzima wa elimu nchini humo ambapo tuliishia katika elimu ya vyuo vya umma. Sasa endelea…

Mnamo mwaka wa 1963, serikali ya Kenya iliahidi elimu ya msingi ya bure kwa watu wake na kwamba ahadi hiyo haikufanikishwa hadi mwaka 2003.

Wananchi walitakiwa kuchangia mfuko wa elimu kwa kulipia ada, kodi na huduma za ajira ambapo baada ya kuchangia, wazazi wengi hawakuwa na fedha za kulipia elimu ya watoto wao hatimaye waliachwa nje ya mfumo wa shule.

Pia, walimu walijikuta wakishiriki katika migomo mara kwa mara kutokana na kutolipwa mishahara yao hivyo kuamua kukusanya ada kutoka kwa mwanafunzi, huku mishahara yao ikishikiliwa hadi ada zote zilipokusanywa.

Watoto wengi walikuwa wanalazimika kuacha shule kwa sababu hawakuweza kumudu gharama hiyo huku pia mara nyingi watoto wakiagizwa nyumbani wakati wa mitihani ya mwisho ili iwe shinikizo kwa wazazi kulipa ada.

Kwa sasa elimu ni bure kama ilivyo hapa Tanzania na kwamba mahudhurio yameongezeka hivyo kuna uhaba wa walimu, madarasa na watoto kutopata masomo yao kwa ufanisi kutokana na ukosefu wa walimu wa kutosha, kitendo kinachosababisha msongamano wa wanafunzi madarasani.

Hayo ni matokeo ya watoto wote wanaohudhuria ambao hapo mwanzo hawakuweza kumudu ada ya shule na watoto wanaotolewa shule binafsi zenye hadhi ya chini ili kujinufaisha na ya elimu ya bure.

Hali hiyo imejenga mahitaji kwa shule binafsi zenya gharama ya chini ambazo wazazi wanaweweza kumudu kulipa ada ili kujifunza katika mazingira yaliyo bora.

Baadhi ya watu wanaamini kwamba msongamano shuleni ni changamoto, kwamba kuna haja ya kuandaa mafunzo ya kiufundi zaidi ili kujenga njia mbadala kwa ajira.

Kenya ilianzisha mfumo wa sasa wa 8-4-4 mwaka wa 1985 ambapo darasa la kwanza hadi la nane ni katika shule ya msingi, darasa la tisa hadi 12 sekondari (kidato cha kwanza hadi nne) na kisha wahitimu kutumia miaka minne chuo kikuu.
Mfumo wa 8-4-4 uliundwa kusaidia wale wanafunzi ambao hawana mpango wa kuendeleza elimu ya juu ambapo umesaidia kupunguza viwango vya wanafunzi wanaoacha shule na kuwasaidia wale wanaoachia shule za msingi kupata ajira.

Ukuaji wa sekta ya elimu nchini Kenya umezidi matarajio baada ya chuo kikuu cha kwanza kuanzishwa mwaka 1970, vingine vitano vilitengenezwa. Mahitaji ya elimu ya juu yamesababisha kuanzishwa kwa vyuo vikuu binafsi.
Vifaa katika baadhi ya vyuo vikuu vya umma ni vya hali ya chini na kwamba wale wa miaka ya juu, hutumwa nyumbani kwa muda ili kuwapa nafasi wanafunzi wageni wanapojiunga na chuo kikuu.

Vyuo vikuu, kama shule za msingi, vina ukosefu wa fedha. Kuna ukosefu wa tarakilishi ya mafunzo na maaabara ni ndogo na hazina vifaa vya kutosha.

Baadhi ya wanafunzi huamua kulipa gharama ya juu kidogo ili kujiunga na vyuo vikuu binafsi kwa sababu hawataki kujihusisha na ushindani wa kutafuta nafasi za kujiandikisha. Pia, vyuo vikuu hivyo huwa na vifaa bora na maabara ya tarakilishi za hali ya juu.

Serikali ya Uingereza inaipatia Kenya msaada wa Sh bilioni saba (Dola milioni 97 za Marekani) kusaidia kuboresha mfumo wa elimu ya bure. Fedha za ziada zitatumika kuboresha mipango ya afya katika shule zote. Pia, zinatumika katika ununuzi wa vitabu vya kusomea.

Fedha hizo zinakwenda pia kupanua elimu ya shule ya upili na vyuo vikuu. Pia kutakuwa na ujenzi wa madarasa na uboreshaji wa vifaa vya maji pamoja na usafi wa mazingira.

Ingawa Kenya ina vyuo vikuu vyake, baadhi ya wazazi huchagua kupeleka watoto wao katika nchi mbalimbali za kigeni. Wengi wanaamini kwamba Uingereza ina vyuo vikuu bora na kwamba itakuwa fursa kubwa kwa watoto wao kuhudhuria chuo kikuu huko.

Vyuo vikuu vya Kenya pia ni vigumu zaidi kujiunga navyo kutokana na mahitaji makubwa ya elimu ya juu na kuwapo kwa nafasi chache kwa wanafunzi kujiunga navyo.

Serikali ya Kenya ingawa kwa mwendo wa kobe, inajizatiti kufanya elimu nchini Kenya kuwa bora zaidi. Miaka 12 ya kwanza ya shule sasa yanatolewa bure, japo hii imechangia suala la msongamano shuleni; jambo linalohitaji kushughulikiwa kwa haraka.

Ufadhili kutoka Uingereza utasaidia kujenga upya baadhi ya shule na hii itachangia kuboresha mazingira ya kujifunza.

Shule za binafsi

Shule binafsi nchini Kenya kwa ujumla huhudumia watu wa tabaka ya kati na ya juu. Nyingi ni ya mashirika ya kidini tofauti tofauti kama vile Oshwal Academy ambayo inamilikiwa na kusimamiwa na OERB (jamii ya Oshwal – Wakenya wenye asili ya Kihindi wanaofuata dini ya Jainism); Katoliki (Saint Mary’s School Nairobi), Wamisionari (Rift Valley Academy) na za Kiislamu (Aga Khan Academy).

Mashirika haya kwa ujumla hufadhili shule hizo, na kwa kawaida hakuna upendeleo wa kidini au wa njia yoyote ile katika kuwachukua wanafunzi na uendeshaji wa shule.

Shule nyingi binafsi nchini Kenya zinapatikana kakita Jiji la Nairobi na Mombasa, huku shule za bweni zikipatikana sehemu ya mashambani au viungani mwa miji.

Hii ni sambamba na mila ya familia za Uingereza za tabaka ya juu na juu ya kati kuwatuma watoto wao shule za bweni za gharama kubwa ambazo zina nafasi ya kutosha na vifaa.

Shule zenyewe zinafanana na shule za umma za Uingereza, huku shule nyingi binafsi jijini Nairobi aidha kuzingatia mfumo wa shule za umma kama Brookhouse School, au kuwa shule za umma chini ya utawala wa kikoloni kama vile Saint Mary’s School, Nairobi na Kenton College.

Uingereza huku shule nyingi binafsi jijini Nairobi aidha, kuzingatia mfumo wa shule za umma kama vile Brookhouse School au kuwa shule za umma chini ya utawala wa kikoloni kama vile Saint Mary’s School, Nairobi na Kenton College.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles