Selena Gomez: Bado nampenda Justin Bieber

0
923

SelenaNEW YORK, MAREKANI

MWANAMUZIKI maarufu nchini Marekani, Selena Gomez, ameibuka na kudai kwamba bado anampenda aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa RnB, Justin Beiber.

Wawili hao walianza uhusiano mwaka 2011, lakini miaka mitatu baadaye waliachana.

Hata hivyo, japokuwa wameachana, lakini mrembo huyo amesisitiza kuwa ataendelea kumpenda msanii huyo kwa kuwa alimzoea na wamekuwa wote tangu wakiwa wadogo.

“Siwezi kuzuia hisia zangu kwa Beiber, nitaendelea kumpenda milele kwa kuwa nilimzoea na nimekuwa naye tangu tukiwa wadogo.

“Tangu tumeachana hakuna mtu ambaye amefanikiwa kuoa au kuolewa, hivyo kwa upande wangu nitaendelea kumsapoti kwa kila hali na mali,” alisema Selena.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here