Christina Gauluhanga, Dar es Salaam
Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), umesema Sekta ya madini inaongoza kwa vifo na ajali kwa sababu ya Mazingira ya kikazi.
Akizungumza na Mtanzania Digital leo Julai 4, katika Maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba (DITF), Mkurugenzi Mkuu wa OSHA, Alexander Ngata amesema uchunguzi uliofanywa umeonyesha sekta hiyo inaongoza kwa matukio hayo tofauti na nyingine.
Ngata amesema baadhi ya sekta mbalimbali zinafanana changamoto za kikazi.
” OSHA imefanikiwa kusajili makampuni machache kwa ajili ya ukaguzi wa hali ya Mazingira na afya ya wafanyakazi wake,” amesema.
Aidha amesema changamoto iliyopo katika maeneo mengine ni kukosekana kwa taarifa sahihi kwa sababu ya mifumo.