25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SBL yatenga Sh bilioni 5 kununua mtama, shayiri

Bia ya Serengeti
Bia ya Serengeti

NA BENJAMIN MASESE, MWANZA

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imetenga kiasi cha Sh bilioni 5.5 ili kununua kwa wakulima mazao ya mtama na shayiri katika msimu ujao kwa ajili ya matumizi ya kiwandani ya kampuni hiyo.

Akizungumza hivi karibuni Jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Bodi ya SBL, Nehemia Mchechu, alisema SBL imeamua kuwa mdau wa maendeleo katika nyanja za kodi, elimu, afya, maji, mazingira na kuendeleza uwekezaji unaonufaisha makundi yote ndani ya jamii.

“Tumeamua kununua mazao hayo ya mtama na shayiri ikiwa ni jitihada za kupunguza uagizaji wa malighafi kutoka nje ya nchi, SBL imekuwa na desturi ya kuwawezesha wakulima kila mwaka kwa kuwapatia mbegu bora bila malipo.

“Katika msimu huu, SBL imetoa mbegu za shayiri zenye thamani ya Sh milioni 600, ndiyo maana tumetenga Sh bilioni 5.5 kwa ajili ya kununua mazao hayo katika msimu ujao.

“Hadi Desemba mwaka jana, asilimia 100 ya bia zote zilizozalishwa na SBL malighafi zake zilikuwa za hapa Tanzania, lengo la kampuni ni kutaka ifikapo 2017 hakuna kufuata malighafi nje ya nchi, ndiyo maana tunawawezesha wakulima kwanza,” alisema.

Alisema lengo na juhudi za SBL ni kusaidia kuongeza ajira, kutoa soko kwa wakulima, kupunguza matumizi ya fedha za kigeni na kuokoa uwezekano wa kuhamishia ajira nje ya nchi.

Mchechu alisema kampuni hiyo ya bia imejipanga kuwakwamua wananchi kiuchumi pamoja na kuchangia juhudi za Serikali za kuinua uchumi wa nchi na kuongeza kwamba utekelezaji na uwekezaji katika kilimo utachangia  sera ya kilimo kwanza kufikia lengo.

Alisema kuwa hivi sasa SBL imeingia mikataba na wakulima wa mikoa na maeneo ya  Kilimanjaro, Basuto, Monduli na Manyara, Njombe, Songea na Rukwa kwa kuwapa mbegu bora, ushauri na kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa lengo la kunufaika na kilimo hicho.

Pamoja na hali hiyo, alisema kampuni hiyo inaendelea na utafiti wa maeneo ambayo yanashawisha zao la mtama na shayiri ili kuwahamasisha wakulima na kuwapatia mbegu bure ili kupata manufaa zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles